.

Alhamisi, 20 Novemba 2014

AFARIKI AKIFANYA MAPENZI KWENYE GARI


Polisi mkoani Kagera inachunguza kifo cha mmiliki wa ukumbi wa klabu ya usiku ya Linas Night, Leonard Mtensa (50) ambaye inadaiwa alifariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye gari lake.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema Mtensa, ambaye alikuwa na mpenzi wake kwenye gari maeneo ya Buyekera, alifariki dunia kabla ya kufikishwa kituo cha afya cha ELCT Ndolage.

Alisema binti waliyekuwa naye kwenye gari anatokea mkoani Mara na kwamba tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana. Alisema baada ya gari lake kupekuliwa, vilikutwa vinywaji mbalimbali.

“Baada ya upekuzi ndani ya gari lake, vilikutwa vilevi vya aina mbalimbali, ikiwamo whisky aina ya Bond 7 aliyokuwa anakunywa, lakini chanzo cha kifo hicho hakijajulikana,” alisema Mwaibambe.

Kamanda Mwaibambe alisema polisi wanamshikilia mpenzi wake kwa ajili ya upelelezi kwa hatua zaidi. Kifo hicho kimeshtua wakazi wa Bukoba, kutokana na mazingira ya kifo cha mfanyabiashara huyo anayemiliki ukumbi pekee mjini hapa unaotoa burudani hadi asubuhi.
SOURCE:MWANANCHI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni