Wakati mwingine watu huenda mbali na kutazama ligi ambayo imetoa timu zenye mafanikio katika michuano ya kimataifa na kuziona kuwa bora japo bado kigezo hicho hakitoshi lakini gazeti moja la Uingereza The Daily Mail limefanya utafiti kwa kuzingatia vigezo kadhaa na katika utafiti huo wameweza kugundua kuwa ipo ligi ambayo ina ubora kuliko ligi nyingine.
Baadhi ya vigezo vilivyotazamwa na gazeti hilo katika utafiti wake ni ushindani wa timu na timu, kipato kwa timu na mishahara kwa wachezaji na makocha, bei za tiketi, mahudhurio ya mashabiki viwanjani, makocha, vipaji vinavyozalishwa, kukuzwa na kuendelezwa, mataji na mafanikio ya uwanjani pamoja na mchango wa ligi husika kwenye mchezo kitaifa.
Kupitia vigezo hivyo gazeti la The Daily Mail limeweza kuzitazama ligi 34 toka kwenye maeneo tofauti duniani kuanzia Afrika, Asia, Australia, Amerika ya kusini na kaskazini pamoja na Ulaya.
Katika utafiti huo ligi kuu ya England maarufu kama EPL ndio imetajwa kuwa ligi bora kuliko zote duniani baada ya kuonekana kukidhi vigezo vyote vilivyotajwa katika utafiti.
Mataji.
Ligi ya England imeonekana kutawala katika mataji ya ulaya baada ya timu za Manchester United , Chelsea na Liverpool zote kutwaa mataji ya ulaya pamoja na kucheza kwenye fainali nyingi za michuano ya Ligi ya mabingwa na UEFA Europa .
Ligi kama ya ujerumani pamoja na ubora inaotajwa kuwa nao imewexza kumtoa bingwa wa ulaya mara moja tu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita huku kukiwa hakuna timu ya ujerumani hata moja iliyoanikiwa kutwaa ubingwa wa uefa europa .
Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita michuano ya ligi ya mabingwa imetawaliwa na timu za England na Hispania ambazo kwa pamoja zimekusanya jumla ya mataji nane ya ligi ya mabingwa ambayo yamegawanywa kwa timu tano za Manchester United , Chelsea , Liverpool , Real Madrid na Fc Barcelona huku zikitwaa taji la uefa Europa mara sita kwa jumla .
Makocha .
Katika kigezo cha makocha ligi ambayo ina mjumuiko mkubwa wa makocha bora imetajwa kuwa ligi ya China ambayo ndio ligi pekee yenye kocha ambaye ameweza kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani ulaya pamoja na kombe la dunia akiwa na timu ya taifa .
Kocha huyu ni Muitaliano Marcello Lippi ambaye hivi karibuni alitangaza kustaafu akiwa na klabu ya Guangzhou Evergrande .
Hata hivyo kwa kutazama ubora wa makocha kwa vigezo vya mafanikio waliyopata ligi ya England inaziacha mbali ligi nyingine kama ya Ujerumani Bundesliga na Hispania .
Ligi ya England ina mkusanyiko wa makocha kama Jose Mourinho na Louis Van Gaal ambao wametwaa mataji lukuki wakiwa na timu kwenye ligi tofauti.
Mdachi
Louis Van Gaal anayefundisha Manchester United ametwaa mataji ya ligi
kuu akiwa kwenye nchi tatu tofauti na timu nne tofauti .
Jose
Mourinho kama Van Gaal ametwaa mataji ya ligi kwneye nchi nne tofauti
akiwa na klabu nne tofauti huku akitwaa pia taji la ligi ya mabingwa
akiwa na timu mbili tofauti .
Uwiano wa Ushindani .
Katika kigezo hiki ligi ya England na Hispania zimeachwa kidogo na ligi ya ujerumani ambayo katika kipindi cha miaka kumi imeshuhudia angalau timu nne tofauti zikitwaa ubingwa wakati kwenye ligi za Hispania , England na Italia ni timu tatu pekee .
Kwenye ligi nyingine ndogo kama Ugiriki , Ureno , Croatia na Ukraine hakuna ushindani kabisa hali ambayo inaonyeshwa na jinsi ambavyo timu moja moja zimefanikiwa kutwaa angalau asilimia 75% ya misimu ya ligi .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni