Siku chache baada ya yule jamaa aliyevunja rekodi ya kutembea kwenye kamba umbali mrefu akiwa amefunga macho kwa kitambaa, leo kuna story ya hawa wengine ambao huenda rekodi yao ikawa ya kipekee pia kutokana na mazingira ambayo walifanikisha zoezi hilo.
Safari hii rekodi hiyo imevunjwa Afrika, ambapo Lukas Irmler kutoka Ujerumani na Reinhard Kleindl
kutoka Austria walifunga safari na kuingia Afrika na kuvunja rekodi
hiyo katika maporomoko maarufu ya Victoria Falls yaliyopo mpakani mwa
Zambia na Zimbabwe.
Unaambiwa wakali hao walimaliza safari
yao juu ya kamba umbali wa mita mia moja, ambayo iliisha salama mbali na
changamoto ya upepo mkali pamoja na nguvu ya uvutano ya maji ambayo
iliwafanya wayumbe lakini kilichowasaidia ni kuangalia mbele muda wote
kitu ambacho hakikuwa rahisi.
Rekodi hii ni ya pili kuingia kwenye headlines, ambapo ya kwanza ilivunjwa Chicago Marekani na Nik Wallenda ambaye alijifunga kitambaa usoni na kutembea umbali wa mita 182 katika kamba iliyofungwa katikati maghorofa mawili marefu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni