
Habari
zilizotufikia kutoka Mwanga Mkoani Kilimanjaro zinasema kuna ajali
mbaya imetokea maeneo ya Mwanga wakati basi la kampuni ya Mbazi
Travellers lililokua likitokea Arusha kuelekea Dar es salaam kupinduka.

Taarifa
kutoka kwa ripota wangu wa nguvu zinasema ajali hiyo ilitokea baada ya
basi hilo kujaribu kulipita basi jingine huku kukiwa hakuna mtu
aliyepoteza maisha lakini inasemekana kuna idadi kubwa ya majeruhi ambao
walikimbizwa katika hospitali ya KCMC Moshi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni