Siku
tatu baada ya kutolewa taarifa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya
Tanzania kuhusiana na safari ya rais Dkt. Kikwete kwenda Marekani kwa
ajili ya kupatiwa matibabu, ipo taarifa nyingine kuhusiana na President
baada ya kutibiwa.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji wa tezi dume baada ya uchunguzi wa
kidaktari kugundua ana tatizo hilo katika Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland Marekani.
Upasuaji huo umechukua saa moja na nusu na umefanyika salama na kwa
mafanikio ambapo sasa hali ya Rais Kikwete inaendelea vizuri japo bado
yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Saa chache zilizopita kupitia ukurasa wa Twitter wa Rais Kikwete (@jmkikwete) Ikulu wameandika >>> “08/11/2014
Mheshimiwa Rais Dkt Jakaya Kikwete alifanyiwa upasuaji wa Tezi Dume
uliokamilika salama katika Hospitali ya John Hopkins. – Ikulu”
Tweet nyingine kwenye Twitter ya President ikasema >>> “Leo
09/11 Mheshimiwa Rais anaendelea vizuri na ameanza mazoezi, tutaendelea
kuwajulisha maendeleo yake na tuungane katika kumuombea. – Ikulu”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni