.

Jumamosi, 5 Julai 2014

WEMA, MAMA YAKE kuwasomea ALBADILI waliosambaza Picha Chafu


SIKU chache zimekatika tangu kusambazwa kwa picha feki inayodaiwa ni ya mama wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu, wawili hao wako kwenye mkakati mzito wa kuwasomea kisomo cha Albadili wale wote waliohusika kwa namna yoyote ile kuitengeneza picha hiyo na kuitupia mitandaoni, Risasi Jumamosi linakumegea.
Picha hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa na kichwa cha mama Wema, lakini sehemu ya kuanzia shingoni kwenda chini si yeye na mhusika alikuwa hana nguo, ilizua gumzo kwa wiki mbili sasa huku watu wanaojiita Timu Dengue wakitajwa kuhusika.
Wema Sepetu ‘Madam’.
Wema Sepetu ‘Madam’.

KINYWANI MWA CHANZO CHA HABARI

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mama Wema na mwanaye wameamua kusoma Albadili ili kuwaadabisha wale wote waliohusika na sakata hilo lenye kufedhehesha.
“Mama Wema na mwanaye walikasirishwa sana na watu waliotengeneza ile picha na kuitupia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram.
“Wiki iliyopita baadhi ya wasamaria wema walikwenda nyumbani kwa mama Wema na kumtajia majina ya wahusika, lakini hawakuwa na ushahidi hivyo yeye na Wema wameamua kujiunga kiimani zaidi kwa kusoma Albadili.
“Wamesema kwanza kabla ya tukio hilo la Abdadili wametoa siku saba kwa yeyote anayejijua amehusika na picha zile za kutengeneza aende mwenyewe kwa mama Wema, nyumbani kwake, Sinza-Mori (Dar) ili kuomba msamaha.
Wema Sepetu akiwa na mama yake, Mariam Sepetu.
Wema Sepetu akiwa na mama yake, Mariam Sepetu.
“Kama zitapita siku saba na hakuna atakayejitokeza, Albadili itasomwa na mmoja baada ya mwingine watakufa. Tayari wameshawasiliana na mashehe ambao watasoma Albadili hiyo,” kilisema chanzo hicho.

WEMA AYEYUKA HEWANI

Baada ya kusikia kutoka kwa chanzo chetu cha uhakika, juzi Risasi Jumamosi lilimsaka Wema ili kumsikia anasemaje kuhusu kuwepo kwa madai hayo lakini muda mwingi wa maandalizi ya habari hii, simu yake haikuwa hewani!

MAMA WEMA SASA

Baada ya kumkosa Wema, Risasi Jumamosi lilimtafuta mama yake, naye kwa njia ya simu na alipopatikana aliombwa kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo.

KUHUSU ALBADILI

Akizungumza kwa hasira huku sauti yake ikionesha dalili kwamba bado hayuko sawa, mama Wema alisema:
“Ni kweli, nimeshapanga kufanya hivyo, nitasoma Albadili. Haiwezekani watu wakae na kuamua kunichafua mimi, nimewakosea nini cha mno mpaka kufikia kufanya vile! Siwezi kukubali hata kidogo.”

KUHUSU MASHEHE

“Ni kweli pia, nimeshawasiliana na mashehe. Wao wako tayari wanachosubiri ni kupita kwa siku ambazo nimetoa. Kama hakuna atakayejitokeza kuomba radhi, kisomo cha Albadili kitasomwa, wataanza kupukutika mmoja baada ya mwingine kweli nasema.”

SIKU SABA ZINAANZA LINI?

“Jumamosi ijayo (leo) itakuwa siku ya kwanza. Kwa hiyo mpaka Ijumaa ya Julai 11 (mwaka huu), itakuwa siku ya mwisho.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni