Mtuhumiwa
wa kesi ya kujeruhi kwa kumng’ata sehemu mbalimbali za mwili
mfanyakazi wa ndani, inayomkabili Amina Maige (42) amepatiwa dhamana
jana baada ya mahakama kuthibitisha kuwa hasira kutoka kwa wananchi
zimepungua.
Hakimu
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Yohana Yongolo alisema
ameridhishwa na ufafanuzi uliotolewa na Mwendesha mashitaka wa Serikali
pamoja na Wakili wa mshitakiwa kuwa haki ya dhamana itolewe kwa kufuata
masharti na kwamba hakuna uhalifu wowote utakaofanyika dhidi ya
mshitakiwa huyo.
Hakimu
Yongolo alitoa masharti ya dhamana ambayo yalimtaka Maige kutoondoka
nje ya Dar es salaam bila ya ruhusa ya mahakama hiyo.
Pia
alitoa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa kutoka taasisi
inayotambulika hapa nchini ambapo mdhamini huyo anaweza kuwa mwajiriwa,
mfanya biashara na mkulima.
Alisema wadhamini hao watatakiwa kusaini hati ya makubaliano kwa kila mmoja kulipa Sh milioni tatu.
Aliongeza kuwa kesi hiyo itasikilizwa Julai 22 mwaka huu.
Maige
alidaiwa Januari mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alimng’ata na kumchoma
na pasi sehemu mbalimbali za mwili wa mfanyakazi waje wa ndani Yusta
Kashinde (20) na kumsababishia maumivu mwilini.
Tupe maoni yako hapo Chini..!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni