.

Jumapili, 23 Novemba 2014

Hatimaye Diamond Aongelea Kuhusu Kuachana na Wema na Mahusiano yake na Zari Boss Lady

Jana Nov 21, Diamond amesikika kwenye show ya XXL ambapo amezungumzia mambo mengi, baadhi ya yale aliyoyazungumzia ni pamoja na story zilizoenea mitandaoni kwamba mahusiano ya msanii huyo na Wema yameisha pamoja na story ambayo imetokana na kuenea kwa picha mitandaoni za msanii huyo na Zari the Boss Lady kutoka Uganda.
Hii ni sehemu ya mahojiano aliyofanya Diamond kwenye XXL:

Adam Mchomvu :”…Nataka kujua ile vibe ya Fiesta that day, story zilikuja ooh Diamond kazomewa.. kazomewa kazomewa..na vitu kama vile, sijapata chance ya kukusikia wewe una kipi cha kuzungumzia kuhusiana na that situation..?“

Diamond :- “… Siku zile kwangu ilikuwa kama mchezo, unajua muziki ushakuwa kama sio fani tena, ushakuwa kama siasa.. So, lazima uichukulie hivyo wewe mwenyewe kama msanii ujue una control vipi kwa sababu sio mara ya kwanza vitu kama hivyo vishatokea Maisha.. Maisha yalitupwa mpaka na mayai viza kabisa.. Ni vitu ambavyo vikitokea naonaga kama ni kawaida…“

B 12  :-“…Kwa hiyo ukweli uko wapi kati yako wewe na Wema Sepetu?…”

Diamond  :- “…Kuna vitu vitu fulani nadhani kuvizungumza sio vizuri… Lakini ikifikia kuvizungumzia vinazungumziwa… Uzuri wa mahusiano yetu ni kwamba kila mtu anafahamu… Haijafikia kuweka wazi ndio maana ninapoulizwa inakuwa ni swali gumu kulijibu.. “

B 12 :- “.. Ni gumu kwa upande wako lakini yeye yuko tayari kuzungumza kwamba it’s over kati yangu mi’ na Diamond…“

Diamond  :- “… Sijui…“

B 12  :- “…Hii ngoma kama umemzungumzia yeye direct hivi… watu wamekuza akili zao zikaenda mbali zaidi kimawazo lakini, kwamba inawezekana ile singo umemwimbia yeye hivi kwamba bado unamzimia japokuwa bado kama kakutosa hivi…“
wemadiamond

Diamond  : “.. Waswahili wanasema ‘A’ na ‘B’ yote majibu, halafu ukisikiliza ile nyimbo kama kweli mtu mwenye ufahamu wako, kweli kabisa hauwezi kuwa na maswali mengi …“
Kuhusiana na mahusiano yake na Zari the Boss Lady, Diamond amejibu hivi:

Diamond  :- “.. Zari ni rafiki yangu tu, alipokuja hapa mimi ndio nilikuwa mwenyeji wake Tanzania na kama mimi ndiyo mwenyeji sikutaka kuleta roho za kibaguzi, unajua hata alipokuja Davido pia ilibidi awe na mimi karibu ili hata kesho na kesho kutwa  mimi nikiwa Nigeria basi Davido anipokee hivyo hivyo…“

Ijumaa, 21 Novemba 2014

Hivi ndivyo Whatsapp imevunja ndoa ya wawili hawa…


whatsapp2Wiki chache baada ya WhatsApp kutambulisha mfumo mpya ambapo iwapo unamtumia message mtu inakuonyesha alama ya tick mbili za kijani na pia inaonyesha muda ambao mtu uliyemtumia message hiyo ameisoma, tayari kuna ndoa ambayo imeingia matatizoni kutokana na hilo.
Mwanaume mmoja Saudi Arabia ametoa talaka kwa mkewe kutokana na kitendo cha mwanamke huyo kutokujibu message aliyomtumia WhatsApp.
Mwanaume huyo amesema kitendo kilichomkasirisha zaidi ni pale aliporudi nyumbani na kumkuta mke wake akiwa busy anachat na marafiki zake kupitia mtandao huo wakati message aliyomtumia yeye hakuijibu.
dreamstime_s_36639295-600x399
Jamaa huyo ameona kama kitendo hicho ni dharau kubwa na hakuwa tayari kuendelea na ndoa hiyo ambayo imedumu kwa miaka miwili tangu ifungwe.

Ronaldo aosha vyombo baada ya kushindwa


Ronaldo aosha vyombo baada ya kushindwa katika karata na mchezaji wa Tenisi Rafa Nadal
Ronaldo aosha vyombo baada ya kushindwa katika karata na mchezaji wa Tenisi Rafa Nadal
Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Brazil Ronaldo alilazimika kuosha vyombo baada ya kushindwa katika mchezo wa karata na mchezaji wa tennisi Rafa Nadal,na kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea dola 50,000 za hazina yake ya kutoa msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alikabiliana vilivyo na mwana tenisi huyo kutoka uhispania katika mechi kati ya wawili hao katika meza ya pokerstar, Casino ya Hippodrome mjini London ambapo Nadal alishinda fedha hizo.
Duru ziliarifu kwamba kiini cha nyota hao wawili kukutana katika chumba kimoja ni chakula kilichoandaliwa katika hafla hiyo.
Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi kulingana na wageni ni hatua ya Ronaldo kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha vyombo vya Nadal alivyotumia kula.

Binti asema hapana kuasiliwa na Kim kardashia

Pink

kim kardashia


Mtoto aliyekuwa akiishi katika mazingira ya umasikini katika Nyumba ya kulea Watoto yatima nchini Thailand amefanya uamuzi wa kushangaza alipokataa ombi la Nyota maarufu duniani Kim Kardashian kumuasili kuwa sehemu ya familia yake.
Taarifa zinasema binti huyo alifurahi sana aliposikia milionea huyo anataka kumuasili, lakini alisisitiza kuwa anataka kusoma nchini Thailand akimtaka Kim kuisaidia nchi yake na watoto wenzake wanaoishi pamoja katika nyumba ya watoto yatima.
Kim alivutiwa na binti huyu aitwae Pink mwenye umri wa miaka 13, alipotembelea nyumba ya watoto yatima katika Jimbo la Phang Nga,eneo ambalo zaidi ya watu 4,000 walipoteza maisha kutokana na Tsunami mwaka 2004.
Pink alipelekwa na mama yake katika nyumba ya kulelea watoto kwa kuwa hakuweza kumlea mtoto huyo na kugharamia elimu yake.
Binti huyu anasema yeye na Watoto wenzake walipokutana na Kim Kardashian hawakumfahamu yeye ni nani.
Pink ambaye jina lake halisi ni Laddawan Tong-Keaw, alifurahi kukutana na Nyota huyo, amesema na yeye anapenda sana kuonekana kwenye Televisheni.
Pink husafiri umbali wa Maili 100 kwa basi na Watoto wenzake wawili kwenda Shule inayoongoza jimboni humo inayomilikiwa na Serikali baada ya kufaulu mitihani yao kuingia shule hiyo.
Binti huyu huamka saa kumi na moja alfajiri na kurejea nyumbani saa kumi na mbili jioni.

Alhamisi, 20 Novemba 2014

AFARIKI AKIFANYA MAPENZI KWENYE GARI


Polisi mkoani Kagera inachunguza kifo cha mmiliki wa ukumbi wa klabu ya usiku ya Linas Night, Leonard Mtensa (50) ambaye inadaiwa alifariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye gari lake.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema Mtensa, ambaye alikuwa na mpenzi wake kwenye gari maeneo ya Buyekera, alifariki dunia kabla ya kufikishwa kituo cha afya cha ELCT Ndolage.

Alisema binti waliyekuwa naye kwenye gari anatokea mkoani Mara na kwamba tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana. Alisema baada ya gari lake kupekuliwa, vilikutwa vinywaji mbalimbali.

“Baada ya upekuzi ndani ya gari lake, vilikutwa vilevi vya aina mbalimbali, ikiwamo whisky aina ya Bond 7 aliyokuwa anakunywa, lakini chanzo cha kifo hicho hakijajulikana,” alisema Mwaibambe.

Kamanda Mwaibambe alisema polisi wanamshikilia mpenzi wake kwa ajili ya upelelezi kwa hatua zaidi. Kifo hicho kimeshtua wakazi wa Bukoba, kutokana na mazingira ya kifo cha mfanyabiashara huyo anayemiliki ukumbi pekee mjini hapa unaotoa burudani hadi asubuhi.
SOURCE:MWANANCHI

Jumatano, 19 Novemba 2014

UMEZIONA PICHA KUMI ZA MUONEKANO MPA WA RICK ROSE HIZI HAPA>>


Bi harusi apewa talaka siku ya harusi


Bi harusi apewa talaka siku ya harusi.Picha niaba ya gazeti la Daily Mirror nchini Uingereza
Bwana harusi mmoja kutoka Saudi Arabia amempa talaka mkewe siku ya harusi baada ya kumuona uso wake kwa mara ya kwanza wakati mpiga picha alipotaka kuwapiga picha.
Maharusi hao kutoka mji wa magharibi wa Saudia,Medinah walikubaliana kuoana licha ya kutoonana uso kwa uso,swala ambalo ni utamaduni mkubwa wa mataifa ya mashariki ya kati.
Lakini wakati mwanamke huyo alipofungua kitambara alichokuwa amejifunika uso na kutabasamu katika kamera,mumewe alishtuka na kuondoka wa ghafla.
Kulingana na gazeti moja katika eneo hilo kwa jina Okaz,mwanamume huyo alianguka na kuzirai huku wageni waalikwa wakijaribu kuingilia kati ili kutatua kilichokuwa kikiendelea.
Hata hivyo Bwana harusi alisema kuwa hakuweza kumwona bi harusi kabla ya harusi yao gazeti hilo la Okaz liliripoti.
'' Si wewe msichana niliyetaka kuoa,si wewe kamwe niliyedhani '' kwa hivyo nakupa talaka''alisema bwana harusi.
Na alipompa talaka bi harusi naye alianguka na kuzirai na kuifanya harusi hiyo kuwa usiku wa majonzi.

Unajua Rekodi ya kwanza iliyovunjwa ya watu kutembea juu ya kamba Afrika?

AVictoria
Siku chache baada ya yule jamaa aliyevunja rekodi ya kutembea kwenye kamba umbali mrefu akiwa amefunga macho kwa kitambaa, leo kuna story ya hawa wengine ambao huenda rekodi yao ikawa ya kipekee pia kutokana na mazingira ambayo walifanikisha zoezi hilo.
Safari hii rekodi hiyo imevunjwa Afrika, ambapo Lukas Irmler kutoka Ujerumani na Reinhard Kleindl kutoka Austria walifunga safari na kuingia Afrika na kuvunja rekodi hiyo katika maporomoko maarufu ya Victoria Falls yaliyopo mpakani mwa Zambia na Zimbabwe.
0
Unaambiwa wakali hao walimaliza safari yao juu ya kamba umbali wa mita mia moja, ambayo iliisha salama mbali na changamoto ya upepo mkali pamoja na nguvu ya uvutano ya maji ambayo iliwafanya wayumbe lakini kilichowasaidia ni kuangalia mbele muda wote kitu ambacho hakikuwa rahisi.
cegrab-20141109-052515-0-1-362x204
Rekodi hii ni ya pili kuingia kwenye headlines, ambapo ya kwanza ilivunjwa Chicago Marekani na Nik Wallenda ambaye alijifunga kitambaa usoni na kutembea umbali wa mita 182 katika kamba iliyofungwa katikati maghorofa mawili marefu.

Jumapili, 16 Novemba 2014

Jamaa wameitaja ligi bora ya soka duniani, nimekuwekea hapa list kamili na vigezo.


the bestMoja ya maswali ambayo wanaolipenda soka duniani wamekuwa wakijiuliza ni kuhusiana na ligi ambayo inaweza kutajwa kuwa bora kuliko zote duniani na ni ngumu kujibu swali hili kwani hakuna vigezo ambavyo moja kwa moja vinafahamika kuwa vinaashiria ubora wa ligi flani kuliko nyingine.
Wakati mwingine watu huenda mbali na kutazama ligi ambayo imetoa timu zenye mafanikio katika michuano ya kimataifa na kuziona kuwa bora japo bado kigezo hicho hakitoshi lakini gazeti moja la Uingereza The Daily Mail limefanya utafiti kwa kuzingatia vigezo kadhaa na katika utafiti huo wameweza kugundua kuwa ipo ligi ambayo ina ubora kuliko ligi nyingine.
_Manchester_City_players_a
Baadhi ya  vigezo vilivyotazamwa na gazeti hilo katika utafiti wake ni ushindani wa timu na timu, kipato kwa timu na mishahara kwa wachezaji na makocha, bei za tiketi, mahudhurio ya mashabiki viwanjani, makocha, vipaji vinavyozalishwa, kukuzwa na kuendelezwa, mataji na mafanikio ya uwanjani pamoja na mchango wa ligi husika kwenye mchezo kitaifa.
Kupitia vigezo hivyo gazeti la The Daily Mail limeweza kuzitazama ligi 34 toka kwenye maeneo tofauti duniani kuanzia Afrika, Asia, Australia, Amerika ya kusini na kaskazini pamoja na Ulaya.
Katika utafiti huo ligi kuu ya England maarufu kama EPL ndio imetajwa kuwa ligi bora kuliko zote duniani baada ya kuonekana kukidhi vigezo vyote vilivyotajwa katika utafiti.
Mataji.
Ligi ya England imeonekana kutawala katika mataji ya ulaya baada ya timu za Manchester United , Chelsea na Liverpool zote kutwaa mataji ya ulaya pamoja na kucheza kwenye fainali nyingi za michuano ya Ligi ya mabingwa na UEFA Europa .
Ligi kama ya ujerumani pamoja na ubora inaotajwa kuwa nao imewexza kumtoa bingwa wa ulaya mara moja tu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita huku kukiwa hakuna timu ya ujerumani hata moja iliyoanikiwa kutwaa ubingwa wa uefa europa .
Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita michuano ya ligi ya mabingwa imetawaliwa na timu za England na Hispania ambazo kwa pamoja zimekusanya jumla ya mataji nane ya ligi ya mabingwa ambayo yamegawanywa kwa timu tano za Manchester United , Chelsea , Liverpool , Real Madrid na Fc Barcelona  huku zikitwaa taji la uefa Europa mara sita kwa jumla .
Makocha .
Katika kigezo cha makocha ligi ambayo ina mjumuiko mkubwa wa makocha bora imetajwa kuwa ligi ya China ambayo ndio ligi pekee yenye kocha ambaye ameweza kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani ulaya pamoja na kombe la dunia akiwa na timu ya taifa .
Kocha huyu ni Muitaliano Marcello Lippi ambaye hivi karibuni alitangaza kustaafu akiwa na klabu ya Guangzhou Evergrande .
Hata hivyo kwa kutazama ubora wa makocha kwa vigezo vya mafanikio waliyopata ligi ya England inaziacha mbali ligi nyingine kama ya Ujerumani Bundesliga na Hispania .
Kocha wa zamani wa Italia Marcelo Lippi.
Kocha wa zamani wa Italia Marcelo Lippi.
Ligi ya England ina mkusanyiko wa makocha kama Jose Mourinho na Louis Van Gaal ambao wametwaa mataji lukuki wakiwa na timu kwenye ligi tofauti.
Mdachi Louis Van Gaal anayefundisha Manchester United ametwaa mataji ya ligi kuu akiwa kwenye nchi  tatu tofauti na timu nne tofauti .
Mdachi Louis Van Gaal anayefundisha Manchester United ametwaa mataji ya ligi kuu akiwa kwenye nchi tatu tofauti na timu nne tofauti .
Jose Mourinho kama Van Gaal ametwaa mataji ya ligi kwneye nchi nne tofauti  akiwa na klabu nne tofauti huku akitwaa pia taji la ligi ya mabingwa akiwa na timu mbili tofauti .
Jose Mourinho kama Van Gaal ametwaa mataji ya ligi kwneye nchi nne tofauti akiwa na klabu nne tofauti huku akitwaa pia taji la ligi ya mabingwa akiwa na timu mbili tofauti .
Ligi ya Ujerumani inafuatia katika kigezo hicho na ligi ya Hispania inashika nafasi ya tatu huku Italia ikishika nafasi ya nne .
Uwiano wa Ushindani .
Katika kigezo hiki ligi ya England na Hispania zimeachwa kidogo na ligi ya ujerumani ambayo katika kipindi cha miaka kumi imeshuhudia angalau timu nne tofauti zikitwaa ubingwa wakati kwenye ligi za Hispania , England na Italia ni timu tatu pekee .
Kwenye ligi nyingine ndogo kama Ugiriki , Ureno , Croatia na Ukraine hakuna ushindani kabisa hali ambayo inaonyeshwa na jinsi ambavyo timu moja moja zimefanikiwa kutwaa angalau asilimia 75% ya misimu ya ligi .
MoS2 Template Master

Mtoto Aliyegeuka nyoka azua balaa Geita


Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi minne amezua kizaazaa cha aina yake, baada ya kuwapo taarifa kwamba mara kadhaa umbo lake limekuwa likigeuka na kuwa nyoka na mwili wake ukiendelea kudhoofu kutokana na kukataa kunyonya maziwa ya mama yake.
Mtoto huyo (jina lake tunalihifadhi kwa sasa), wiki iliyopita alivuta umati wa wakazi wa Kijiji cha Nkome mkoani Geita ambao walifurika ndani na nje ya Kanisa la AICT Nkome, lililopo kijiji hapo, kushuhudia maombi ambayo alikuwa akifanyiwa ili kumkomboa katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni mateso dhidi yake.
Ilikuwa saa 4.00 asubuhi Jumamosi, Novemba 8 mwaka huu wakati mtoto huyo alipofikishwa katika kanisa hilo na kuanza kufanyiwa maombi na sababu ya hatua hiyo ikielezwa kuwa ni kutokana na kuwa na umbo la nyoka na kwamba matendo yake yanaashiria kwamba mwenye asili ya nyoka ndani ya roho yake.
Mtoto huyo alifikishwa kanisani hapo na mama yake mzazi, Sarah Silasi wakitokea Kijiji cha Ichile, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, ambako alikimbia matukio yanayohusishwa na ushirikina.
Mmoja wa wazee wa kanisa hilo la AIC Nkome, Mathew Misana anasema: “Alikuwa anatoa ulimi mithili ya nyoka, mwendo wake anapolala alijizungusha kama nyoka na hata alipojikunja mwili wake ulikuwa kama unavyoona nyoka.”
Misana anasema matukio hayo na mengine kadhaa yakiwamo ya ngozi ya mtoto huyo kuwa nyeusi kama ya nyoka aina ya chatu, yaliwalazimisha ndugu na jamaa zake wakiongozwa na mama mzazi kutaka aombewe.
geita
“Ngozi yake kuonekana kama ya mzee huku macho yake yakionekana kuwa makubwa na kichwa chake kuwa na umbo la nyoka pamoja na miguu, baada ya kuona hali hii tukaihusisha na mambo ya kishirikina na kuamua kuanza maombi,” alisisitiza.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya maombi kuanza, taarifa za kuwapo kwa aina hiyo ya mtoto zilisambaa haraka na kusababisha umati mkubwa wa watu kujaa ndani ya kanisa hilo ambalo ni boma kwa maana kwamba ujenzi wake bado unaendelea.
“Watu wengi walijaa na wengine wakawa wanapanda juu ya miti na juu ya boma wakati mwingine matofali yalianguka. Hewa ikapungua na usalama ukawa mdogo kwani watu walisukumana wakitaka kushuhudia,” anasema Misana.
Baada ya watu kuwa wengi, uongozi wa kanisa uliomba msaada wa Polisi wa Kituo cha Nkome ambao walifika kanisani hapo na kushauri mtoto huyo aonyeshwe ili watu waweze kuridhika kwamba hakuwa amegeuka kuwa nyoka.
Uongozi wa kanisa ulifanya hivyo lakini mwonekano wa mtoto huyo ulisababisha watu kuongezeka badala ya kupungua na hapo ndipo polisi walipoelekeza mama wa mtoto huyo ambebe na kuondoka naye hadi kituoni.
Mwinjilisti wa kanisa hilo, Emmanuel Misungwi anasimulia: “Tumeshudia vitu visivyo vya kawaida wakati tunafanya maombi na wakati tunaendelea na huduma, mama wa mtoto Sarah alianguka akaanza kuongea juu ya mtoto kwa nguvu ya mapepo.”
Anasema hali hiyo iliwavuta watu wengi kiasi cha usalama wa mtoto kuwa mdogo, ndipo walipoamua kuomba msaada wa ulinzi kutoka polisi.
“Ilibidi polisi waingilie kati, walimchukua mtoto na kuondoka naye na kuwaridhisha wananchi kwa kumwonyesha hadharani ili kila mtu aone kama kweli ni nyoka kama uvumi ulivyokuwa umeena au la,” anasema Misungwi.
Kituo cha polisi
Baada ya mama huyo na mwanaye kufikishwa polisi, umati wa watu ulihamia katika kituo hicho na kuwafanya askari kufanya kazi ya ziada kuwaondoa watu waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo.
Licha ya wananchi kufukuzwa waliendelea kun’gang’ania kukaa katika kituo hicho, hali ambayo ilisababisha polisi kumwondoa mwanamke huyo kwa kificho na kumpeleka nyumbani kwa mchungaji wa kanisa hilo, Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Jonh Marko.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nkome, Charles Belenge alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa hali hiyo imesababisha vurugu wakati wa maombi.
“Nikweli tukio hilo lipo la kudai mtoto anabadilika kuwa nyoka, kwa kweli limetupa shida kwani hali ya utulivu katika kijiji ilibadilika kwa muda, lakini tumejitahidi kufanya udhibiti,” anasema Belenge.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba walikuwa wakilifanyia uchunguzi wa kina.
“Haya mambo ndiyo yanasababisha mauaji ya mapanga, hivyo kama Jeshi la Polisi tutafuatilia kujua kwa kina ili lisije kusababisha madhara ya mauaji ya kukatana kwa mapanga,” alisema Konyo.
Alihusisha tukio hilo na uelewa mdogo wa wazazi na wachungaji waliokuwa wakifanya maombi na kwamba mtoto huyo huenda alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya utapiamlo, tofauti na mawazo kwamba tatizo ni nguvu za giza.
“Kazi tunayoifanya kama Jeshi la Polisi ni kuweka ulinzi kwa kuzuia wasifanye maombezi eneo la kanisa hilo ambalo kiukweli liko wazi sana kwani usalama utakuwa mdogo pia tuombe wanaohusika wampeleke mtoto hospitali,” alisema Konyo.
Mashuhuda wa maombi
Misana anasema wakati wakifanya maombi mtoto huyo alikuwa hatoi sauti isipokuwa alikuwa anatoa ulimi kama ufanyavyo nyoka na kwamba ulimi huo ulikuwa mrefu mpaka shingoni pamoja na macho yake kuwa makubwa.
Mashuhuda wengine walisema kuwa waliona mtoto huyo akigeuka kimaajabu na kuwa na maumbo mithili ya nyoka na baadaye kurudi katika umbo la binadamu.
“Mimi nimeona wakati anaombewa alikuwa anatoa ulimi kama nyoka, alikuwa anasimamisha kichwa na kutoa ulimi hadi unagusa shingo halafu tumbo, miguu na kiuno vilizunguka,” anasimulia mkazi wa Nkone, Shaban Masembe.
Naye Neema Masatu anasema: “Niliambiwa Kanisa la AIC kuna mtoto anabadilika kuwa nyoka anafanyiwa maombi ikabidi nije nijionee, nimefika hapa nikakuta kweli watu wamejigawa makundi mawili; wengine wanamuombea mama wa mtoto na wengine mtoto.”
Masatu anafafanua kuwa alichokiona si nyoka isipokuwa ameona mtoto huyo akiwa anatembea kama nyoka, anajikunja miguu inagusa shingo kisha kichwa anakisimamisha kama nyoka na kutoa ulimi mrefu na mdomo na macho yake yalikuwa yanakuwa makubwa.
Naye Pili Nyachimb’huga anasema: “Sijaona, watu walikuwa wengi nimefika hapa hata sikuweza kumuona ila watu wanasema alikuwa mtu anayefanana na nyoka, alikuwa anaachama kama nyoka na kwamba alikuwa anatanuka mwili wake unakuwa mkubwa”.
Ni ipi historia ya mtoto huyu? Usikose toleo lijalo ambapo mama mzazi atazungumzia kwa undani sababu za mtoto wake kuwa na matendo yanayofanana na ya nyoka.

DJ TASS AWAFURAHISHA WABONGO KWA KUPROMOTE MUZIKI WA NYUMBANI NDANI YA BBA HOTSHOTS

Dj Tass wa Majic Fm na Maisha Magic ya DSTV Ijumaa (Nov. 14) alikuwa official Dj aliyetumbiza kwenye jumba la Big Brother Africa Hotshots jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Tass
Mashabiki wengi wameonekana kufurahishwa na uzalendo aliouonesha kwa kupromote zaidi ngoma nyingi za wasanii wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla katika platform ambayo inaonekana kwenye nchi nyingi za Afrika.
Dj Tass aliyekuwa amevalia T-shirt nyekundu yenye picha za Nyerere na Mandelea, ameiambia Bongo5 kuwa alipewa maelekezo ya kucheza nyimbo za Afrika tu.
“Wamekubali sana, baadhi ya watu wa Channel O nimeongea nao kuhusu muziki wa Bongo kwanini haupati airtime wanasema zingine hawafahamu. Lakini tumepata mawasiliano nao tuweze kuwa nawatumia labda muziki wanachambua ni muziki gani ambao wanaweza wakaucheza kwasababu hata mimi jana nimepewa limit nisicheze nyimbo za nje nicheze nyimbo za Afrika tu, kidogo kama walitaka kunipa wakati mgumu nikajipanga upya tena wakanipa hard disc yao nikaweka kwenye hard disc yao nilivyomaliza nikawaachia ili wabaki wanajua muziki gani ambao nimecheza kwa faida yao.“
Tass aliendelea,
“Vile vile nimehojiwa na Channel O ambayo itaweka kwenye website yao kuhusiana na awards za Channel O. Wameniuliza nani unaona anaweza akachukua, nikasema mi nadhani anaweza akachukua Diamond kwasasabu ni mtu wetu.”
Tass-2
Hizi ni baadhi ya nyimbo zilizokuwa kwenye playlist ya Dj Tass iliyowarusha House mates wa Hotshots jana:
1.Alikiba – Mwana
2. Diamond ft. Davido –Number 1 Remix,
3.Lady Jay dee- Joto Hasira
4. Nay Wa Mitego – Nakula Ujana
5.P-Unit – Una (Kenya)
6.Godzilla –Nataka
7.Juma Nature – Hakuna kulala
8.Yamoto Band – Niseme
9.Majirani – Ndo hivyo kunaendaga (Kenya)
Hizi ni baadhi ya comments za mashabiki kuhusu Dj Tass alivyoupromote muziki wa nyumbani kwenye BBA:
shilolekiuno-@djtass kaka wew ni nyoooookoo coz umejua kuipenda nchi yako na hizo ngoma zako kali!! @bigbrother africa oyooooooo
djebrah-Kila Mtu Anamwaga Sifa Kwako, Hiyo Inaonyesha Wazi Ulichokifanya Kimekubalika, Asie Mwaga Sifa Kwako Na Kukosoa Huyo Ni Mchawi, Baadhi Ya Waliodis Ni Wale Wabongo Wasiopenda Vya Home, Wanapenda Vya Nje Ya Home, Sio Wazalendo, Ki Ukweli Umepiga Kazi Nzuri Sana, Umeiwakilisha Vizuri Tanzania na East Africa Kwa Ujumla, Hadi Tshirt Uliyovaa Umeonyesha wazi wewe ni Mzalendo, hujaenda Kuuza Sura, umeenda Kuiwakilisha Nchi Yako, BIG UP SANA SANA SANAAAA DJ TASS.
sharogangstar_genius-Nilikipenda Sana alichokifanya Jana DJ TASS
ndani ya jumba la Big Brother Africa # Hotshots ,Alionyesha Uzalendo Uliotukuka,maana alicheza ngoma nyingi sana za kibongo. . huku akigusa na za Ki East Africa Kenya na Uganda I mean, Alizipa Muda kimtindo pia Zile Naija na Kwaito… Kuna Dj wa kibongo alishawahi kwenda akaishia kucheza ngoma za wenZetu tu, hakugusa ngoma ya bongo hata moja zaidi ya video ya aliyekuwa mshiriki wa humohumo akiwakilisha TZ, Feza kesi . iliniumaga sana kukosa uzalendo wa nyumbani …. Na ahsante waliomvalisha T-shirt iliyokuwa na picha mbili ya Nyerere na Mandela zilizoungana na kuchora ramani kama ya Africa , huku maandishi yakisomeka AFRICAN HEROES….. ulitishaaaaaaa DJ TASS. Moja kati ya status yangu niliyoiandika leo @djtass
foncethomas-Yeah salute kwake kairusha sana nchi
chichimishi-kanichekesha kweli jamani yani BBA leo kama Maisha Club. Hadi Yamoto Band.
abuujunior-Mwaka huu kweli wamepeleka #DJMtanzania
maryyarot-Kabisa yani ameutendea haki u Tanzania wake @abuujuniour
seycelela_msamba-akija wa nigeria watapiga zao wa south vilevile.. by the way aliekwambia utamu wa nyimbo mpaka uelewe maneno nani?? @ djtass umeuaa baba u nailee t.. @shilolekiuno huyu msambazie upendo naona kajisahau
dvjcon-@shilolekiuno dada umeongea umeonaeeee yaan @djtass kanikosha vilivyo kwa kuilitangaza soko la Tanzania kwa kupiga nyimbo za bongo big up @djtass
nurujw-Mbona si tunacheza makirikir kwan tunaelewa tayo kacheza mwanzo mwisho afu umeona nyimbo ya kiba ilivyowanyanyua kwan wanaelewa wabongo tuache mane no lol

Jumamosi, 15 Novemba 2014

PICHA ZA MWANADADA JAY DEE AKIWA LOCATION ANASHOOT VIDEO YAKE MPYA>>>>>PICHA ZOTE HAPA>>>










Majibu ya Shilole kwa shabiki aliyekosoa nyimbo za Bongo kuchezwa sana jumba la Big Brother Africa

.
.
Dj Tass kutoka Tanzania usiku wa November 14 2014 aliiwakilisha Tanzania baada ya kupewa mwaliko wa kwenda kuwarusha  washiriki kwenye jumba la shindano la Big Brother Africa 2014 ambapo sehemu kubwa ya hits alizozicheza ni nyimbo za bongofleva.
Miongoni mwa watu walioangalia burudani hiyo ni Shilole ambaye aliisifia burudani ya Dj Tass kupitia Instagram na kuandika ‘@djtass kaka wew ni ny**o coz umejua kuipenda nchi yako na hizo ngoma zako kali!!@bigbrother africa oyooooooo’
ShiloleBaada ya Shilole kuandika hayo alitokea mmoja wa followers wake ambae aliandika ‘kaitangaza nchi yetu vizuri ila bba it’s all about Africa kwahiyo kwa upande mwingine kawaboa nchi zingine na hata housemates wengine walikua hawachezi maana hawaelewi, kwaio angepiga nyimbo ili wote wafurai,sio sisi tu na idris
Shilole hakuchukua time na akaamua kumjibu shabiki huyo kwa kumuandikia comment hii >>> ‘Utakuwa hauna shukran we dada masna asingepiga pia nyimbo zetu pia ungechamba kama si kuha*****! Dj kapiga nyimbo za nchi zote zilizipo pale, hivi lini mtaacha ushamba wa kukoment ××××× kwani lazima ukoment! Mnaboa, nina wasiwasi wewe utakua sio Mtanzania
.
.
.
.
.
.

Ajali nyingine ya kuanguka kwa jengo la Ghorofa Tano



emergency-sign
Taarifa iliyonifikia muda mfupi uliopita inahusu ajali ya kuanguka kwa Jengo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa.
Mtu mmoja amefariki na wafanyakazi na wakazi wengine wa eneo la Ruaraka, Kenya wamenusurika kifo kutokana na ajali ya kuanguka kwa jengo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa, kwa mujibu wa mashuhuda wanasema ajali hiyo imesababishwa na nyufa zilizokuwa katika jengo hilo.
Taarifa ya Citizen News imesema wakazi wa eneo hilo wamesema kwamba waliwahi kuwakemea wamiliki wa jengo hilo kwa kufanya ujenzi chini ya kiwango lakini hakuna mabadiliko yaliyowahi kufanyika.
Uchunguzi unafanyika kubaini sababu iliyopelekea ajali hiyo.
Wakazi wa eneo hilo wakiwa eneo la tukio lilipoanguka jengo hilo. Picha: Citizen News
Wakazi wa eneo hilo wakiwa eneo la tukio lilipoanguka jengo hilo. Picha: Citizen News

Umesikia kuhusu mwanamke aliyekaa Mochwari kwa saa 11?

jokofuuuuuuuuuu
Story za maajabu ya ulimwengu zinaendelea kukaa kwenye headlines kila siku, na inaponifikia cha kwanza ninachokifanya ni kukufikishia mapema iwezekanavyo ili na wewe usipitwe.
Ya leo inaweza kuwa moja kati ya zilizowahi kukushangaza zaidi, inahusu mwanamke Janina Kolkiewicz raia wa Poland, mwenye umri wa miaka 91 ambaye amekaa kwa muda saa 11 katika chumba cha kuhifadhia maiti huku mwili wake ukiwa ndani ya jokofu baada ya kuthibitishwa na daktari wa familia yake kwamba amefariki, muda mfupi baadaye wahudumu wa mochwari waligundua kwamba ni mzima baada ya kuhisi anatikisika ndani ya mfuko alimowekwa.
Baada ya kurudi nyumbani kwake akitokea mochwari, alilalamika kuhisi baridi kali na kupatiwa bakuli la supu ya moto na mkate.
Daktari aliyethibitisha mauti ya mtu huyo anasema hata yeye anashangazwa na tukio hilo kwani vipimo vyote vilionyesha kuwa mapigo ya moyo yalisimama na hakuwa hai.
Taarifa za kuwa hai mwanamke huyo zilimshtua kila mtu kwenye familia yake na kujikuta ikibatilisha hati ya kifo iliyotolewa kwa ajili ya mazishi yake ambayo yalipangwa kufanyika siku mbili baadaye..

Ijumaa, 14 Novemba 2014

Huwa unaweka vocha kwenye simu na inakwisha upesi? serikali imeongea leo

DSC05550Watumiaji wengi wa huduma ya simu za mkononi wamekuwa wakilalamikia wizi wa pesa unaofanywa na baadhi ya makampuni hayo, leo katika kikao cha Bunge Dodoma Serikali  imesema inatambua kuhusu wizi unaofanywa na baadhi ya makampuni ya simu za mkononi na kutoa tamko namna ambavyo imejipanga kukabiliana na wizi wa aina hiyo.
Akitoa tamko hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba amesema Serikali itaanzisha kituo maalum cha kushughulikia malalamiko hayo CCC, kitakachokuwa kinasimamiwa na TCRA.
Akiuliza swali kuhusiana na jinsi Serikali ilivyojipanga  kukabiliana na wizi huo Mbunge wa Konde Khatib Said Haji amesema; “… Wizi huu unaofanywa na makampuni ya simu si wizi mkubwa kama ule wa ESCROW..  ni wizi mdogo mdogo unaowaibia Watanzania elfu tano elfu tatu lakini kwa ujumla wake, Mpemba aliyeko Konde akiibiwa elfu tatu, Mnyamwezi wa Tabora elfu mbili, Ukizijumlisha ni mamilioni ya shilingi wanaibiwa Watanzania… Leo watu hao elfu tatu elfu mbili unawaambia wapeleke malalamiko yao, gharama hiyo umeikadiriaje hata mtu huyo akadai malalamiko ya elfu tatu..
.. Hivi serikali yenu makini imekuwa wapi muda wote mpaka kukiri kama Watanzania wamekuwa wakiibiwa na bila wenyewe kujijua?, na bado hamna hatua mlizozichukua, ni nani aliyeko nyuma ya pazia hili la kuibia Watanzania na ninyi mkaridhia ama ni yale yaliyosemwa kama CCM ina fund katika wizi huu..?”- Khatib Said Haji.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba amesema; “…Napenda nikiri tatizo la wizi au dhuluma kwa wateja lipo na ndio lililopelekea tukaweka hizi kanuni ambazo zinaweka adhabu na hatua za kuchukua katika kuchukua katika kudhibiti wizi huo.. Licha ya utaratibu wa kawaida wa kulalamika katika makampuni  ya simu, kwa sababu moja ya matakwa ya sheria ni kwamba kampuni za simu zinapaswa kuweka utaratibu wa kuhudumia watekja wake, lakini tumebaini kwamba utaratibu huo una matatizo, unaweza ukapiga  simu muda mrefu isipokelewe, unaweza kuambiwa usubiri na wakati unasubiri kulalamika pia unakatwa..
Kwa hiyo Serikali inafahamu hilo, pamoja na hatua tulizozichukua ni kuweka ule mtambo wa kufuatilia mawasiliano ambao moja ya kazi yake sio kufuatilia tu mapato lakini ubora wa mawasiliano.. Kwa kutambua kuwa makampuni ya simu haya wakati mwingine yanachelewa wakati mwigine yanapuuza wateja, kituo hiki ambacho tunakianzisha namba zake zitasambazwa kila mtu atakuwa nayo, kwa hiyo huna haja kusafiri kufuatilia shilingi elfu mbili elfu tatu elfu tano. Kutakuwa na namba ambayo ni bure kupiga..”- January Makamba.
Kila utakapopiga kulalamika utapewa namba maalum ya lalamiko lako, na lisiposhughulikiwa hata kitengo cha kampuni ya simu kutoshughulikia lalamiko lako na yenyewe itakuwa sababu ya makampuni hayo kuadhibiwa..”- January Makamba.
Unaweza kusikiliza majadiliano juu ya suala hilo hapa kama ilivyokuwa katika kikao cha bunge leo Dodoma.

Taarifa nyingine kuhusu ajali ya basi leo eneo la Mwanga


MWANGAHabari zilizotufikia kutoka Mwanga Mkoani Kilimanjaro zinasema kuna ajali mbaya imetokea maeneo ya Mwanga wakati basi la kampuni ya Mbazi Travellers lililokua likitokea Arusha kuelekea Dar es salaam kupinduka.
Ajali IITaarifa kutoka kwa ripota wangu wa nguvu zinasema ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo kujaribu kulipita basi jingine huku kukiwa hakuna mtu aliyepoteza maisha lakini inasemekana kuna idadi kubwa ya majeruhi ambao walikimbizwa katika hospitali ya KCMC Moshi.
Ajali III

Tazama picha za mtu mrefu zaidi na mtu mfupi zaidi Duniani walipokutana kwa mara ya Kwanza.


Tall IV




Tall III
Tumekuwa tukisikia rekodi mbalimbali zikivunjwa na watu duniani na rekodi hizo maalumu huwa zinatunzwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Guiness World Records.
Kwa mara ya kwanza, watu ambao wako katika kitabu hicho kutokana na kuvunja rekodi hizo za kipekee wamekutana London Uingereza siku ya Novemba 13.
Chandra Bahadur Dangi mtu aliyevunja rekodi ya kuwa mtu mfupi kuliko wote Duniani amekutana kwa mara ya kwanza na Sultan Kosen, jamaa ambaye amevunja rekodi ya kuwa mtu mrefu zaidi duniani.
Chandra anatokea Nepal ana urefu cha Sm. 54.6, Sultan anatokea Uturuki ana urefu wa Sm. 251 ambayo ni sawa na futi 8.3.
Hizi ni picha zinazowaonyesha wakali hao wakiwa pamoja.
Tall II
Tall & Short
Tall III
Tall V

January Makamba kwenye Twitter baada ya kuandikwa na gazeti la Mtanzania


JayMakamba


Kibanda & J Makamba
Gazeti la Mtanzania leo Novemba 14 limeandikwa kichwa cha habari kinachosomeka hivi; “.. Utafiti watibua wagombea urais 2015.. January aupinga, Zitto amwambia aache siasa.. Keissy ashangaa Wasira kutosomeka katika ripoti..”
Kupitia mtandao wa Twitter, hiki ndicho kilichoandikwa na mhariri Absalom Kibanda na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba;
J. Makamba  : “ Unaelezeaje suala la gazeti lako kunukuu kinyume kabisa na mtu alivyosema? Umeambiwa.
A. Kibanda    : “ Nimeambiwa kaka. Badala ya kuandika JM kahoji wao wakaona umepinga utafiti.”
J. Makamba  : “ Si kweli. Na nimesema specifically sipingi. Heshima ndogo niliyobakiwa nayo na Mtanzania imeisha.”
A. Kibanda    : “ You judge the paper kwa kosa ambalo msingi wake ni kauli yako?! Worldwide media zinafanya makosa hayo ya tafsiri”
J. Makamba  : “ makosa yanatokea, ni kawaida na yanasameheka. Kupindisha makusudi kwa malengo mahsusi ni dhambi kwa wasomaji, tasnia na mhusika”
A. Kibanda    : “ Kaka unless silijui hilo. Siwezi kuruhusu gazeti naloongoza likuhujumu wewe au mwingine yeyote. Hata awe Membe anayenichukia”
JayMakamba IV
JayMaka Mwisho

Taarifa kuhusu ajali nyingine ya moto Dar.

Huu ni mfano wa Gari la Kikosi cha Zimamoto.
Huu ni mfano wa Gari la Kikosi cha Zimamoto.
Taarifa zilizotufikia muda mfupi uliopita ni kuhusu tukio la ajali ya moto Dar es salaam.
Kupitia kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds,mtangazaji Adam Mchomvu ametoa taarifa kuhusiana na jali ya moto iliyotokea katika jengo la Machinga Complex lililopo Ilala, Dar es saalam
Chanzo cha moto huo mpaka sasa hakijafahamika na tunaendelea kufuatilia ili kukupa taarifa zaidi na hizi ni baadhi ya picha za tukio hilo.
IMG-20141114-WA0003
IMG-20141114-WA0004 IMG-20141114-WA0005
IMG-20141114-WA0008

Tags :