Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.
Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.
Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila
siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na
kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari.
Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande
mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu
wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu
wapenda ngono.
Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika.
Twende pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO.
Watu wenye pupa za kufanya mapenzi
hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za
kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa
mara kwa mara.
Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.
Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi
kunatajwa kujitokeza kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile
zile za mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile
kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa
mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama hawezi tena
kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA.
Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara
huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo
mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo
kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo
la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa wakati gani?
Watu wanaojiendekeza katika kufanya
mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao kila wanayemtazama barabarani
humtamani bila kujali hadhi yake.
Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao
hata kwa watumishi wa ndani au kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa
kwa vile akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.
Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara
kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka siku
mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi.
KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO.
Raha ya tendo hutegemea sana hisia
iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi, hivyo
basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa
tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.
Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!
KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI.
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.
Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa
wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke.
Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za
kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.
Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.
KUPATA MAGONJWA.
Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya
mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi
holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi,
lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa
wanawake huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri
kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana na
hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka
ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.
Mtete Focus Blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni