Vinara wa Ligi Kuu, Simba wanafahamu kwamba, watani zao Yanga wanawasubili kwa hamu wafanye makosa tu wawashushe kileleni.
Simba leo watashuka kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kuwakaribi Tanzania Prisons kwa lengo moja tu la
kupata ushindi ili kuendelea kubaki kileleni.
Mahasimu wao wakuu, Yanga ambao pia
leo watateremka Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kumenyana na Kagera
Sugar, wapo katika nafasi ya nne na pointi zao 12.
Hiyo ina maana kwamba kama Simba
itavuna pointi tatu au sare itaendelea kukaa kileleni, lakini kama
itapoteza na Yanga kushinda na kufikisha pointi 15 itakuwa imekiweka
rehani kiti chake cha uongozi, kwa vile hatima hatma yao itaamuliwa na
kigezo cha uwingi wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Pia, Simba inafahamu madhara ya
kupoteza mchezo huo hasa baada ya kusakamwa kwa karibu na Azam FC na
Mbeya City ambazo kila moja imejikusanyia pointi 14 na kama zitashinda
mechi zao zijazo zitakuwa na fursa ya kukaa kileleni.
Kocha wa Simba Abdalah Kibadeni
‘King’ alisema: “ Tupo tayari kwa ajili ya kuikabili Prisons, kwa
vyovyote vile mchezo utakuwa na ushindani mkubwa lakini tumejiandaa kwa
ajili ya kuhakikisha tunaibuka washindi.”.
Naye Kkocha wa Yanga,Ernest Brandts
alisema: “Wachezaji wangu wote wapo katika hali nzuri wakiwa na morali
kubwa ya kuhakikisha wanashinda.” Kwa upande wake, Kocha wa Prisons,
Jumanne Chale alisema: “Simba ni timu ya kawaida kama zilivyo timu
zingine,
hatuihofii wala kuigopa, baada ya dakika tisini nina uhakika matokeo mazuri yatakuwa upande wetu”.
Kocha Msaidizi wa Kagera, Mlage
Kabange alisema: “Nadhani hakuna namna ambayo Yanga wataepuka kipigo,
vijana wangu wamepania kuendeleza ubabe kama ilivyoku wenye Uwanja wa
Azam Complex vibonde wa ligi hiyo, Ashanti United wataivaa Coas tal
Union.
Mtete Focus Blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni