Tarehe 9/10 kabla hajalala mwigizaji
Lulu aliwaonyesha mashabiki zake picha ya tatoo yake mpya ambayo
imechorwa juu ya kifua karibu na bega ikiwa ni picha aliyoipost na
ikaambatana na maneno yafuatayo.
“Kumekuwa na kawaida ya watu kuongea
na kuhukumu wenzao bila ya kujua wanachokiongelea pengine!! kwa upeo
wangu mdogo nafahamu sisi wote ni binadamu na tunamtegemea mtu mmoja
MWENYEZI MUNGU…lakini cha kushangaza kuwa watu wako busy kuhukumu wenzao
kuliko hata huyo mwenye cheo chake, hivi Mungu angetaka kufanya kama
wanadamu tunavyofanya tungeangaliana kweli? nadhani umefika wakati wa
kumuachia mwenye majukumu yake kufanya kazi…tuache kujipa u busy usio wa
lazma….!!!ONLY GOD CAN JUDGE ME….Gud nyt fam”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni