MAHAKAMA ya Rufaa Oktoba 30 mwaka huu inatarajiwa kufanya kusikiliza marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viki maarufu kama Babu seya na wanawe. Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na mwanawe pamoja na wakili wao Mabere Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.
Marejeo
hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa mahakama hiyo
ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati. Katika
hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010,mahakama hiyo iliridhia hukumu ya
kifungo cha maisha kwa Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza huku
ikimuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis
Nguza.
Juni
25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu, Dar es
Salaam,iliwatia hatiani Babu Seya na wanawe Papii Nguza ‘Papii Kocha’,
Nguza Mbangu na Francis Nguza kwa kupatikana na hatia ya kubaka na
kulawiti.
Januari
27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas
Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa
na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Addy
Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa
nayo Juni 25 mwaka 2004.
Babu
Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri
kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa
kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya
Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam.
Mtete Focus Blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni