.

Jumatatu, 11 Agosti 2014

Watu wa mashariki mwa Afrika wakabiliwa na uhaba wa chakula


Zaidi ya watu milioni 14 katika eneo la mashariki mwa Afrika wanahitaji msaada wa chakula kutokana na uhaba wa mvua na mizozo mbalimbali, miaka mitatu tangu kutokea ukame uliokithiri kwenye ukanda huo.
Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu utoaji wa misaada ya kibinaadamu-OCHA, mashariki mwa Afrika, Matthew Conway amesema hali ni ya mashaka. Grace Kabogo amezungumza na Mratibu wa Ushirikiano wa OCHA, Luluwa Ali, ambaye kwanza anaanza kuelezea jinsi shirika hilo lilivyojiandaa kukabiliana na tatizo hilo. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Grace Patricia Kabogo
Mhariri: Josephat Charo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni