.

Jumapili, 31 Agosti 2014

Vikosi vya Iraq vyawakabili wapiganaji.




Wapiganaji wa kikurdi
Jeshi la Iraq likishirikiana na wanamgambo wa madhehebu ya ki-shia pamoja na wapiganaji wa ki-kurdi limeanzisha mashambulizi makali ili kujaribu kuwakabilia wapiganaji wa Islamic state ambao wameuzunguka mji wa Amerli.
Wakati huohuo idara ya ulinzi nchini Marekani imesema kuwa ndege za kijeshi za marekani imeangusha misaa ya kibinaadamu katika mji wa Amali uliozungukwa na islamic state.
Maelfu ya watu wamekwama katika mji huo kwa takriban miezi miwili ijapokuwa imebainika kwamba idadi hiyo huenda ikawa ndogo ya inavyokadiriwa.
Duru kutoka mji wa Tuz Khormutu zimeiambia BBC kwamba vikosi vya muungano vinashambulia kutoka kusini na kazkazini.
Ndege ya kijeshi ya marekani
Zimesema kuwa ndege za wanajeshi wa Iraq zinasaidia katika oparesheni hiyo na kukana kwamba ndege za marekani zinahusika.
Zimeongezea kuwa oparesheni hiyo hailengi kuwaondoa wapiganaji hao pekee bali pia inajaribu kuifungua barabara kuu kati ya Baghdad na kazkazini mwa taifa hilo.
Wakati huohuo wanajeshi wa Marekani wametekeleza mashambulizi zaidi ya angani dhidi ya wapiganaji wa Islamic state karibu na bwawa la Mosul kazkazini mwa Iraq.
Idara ya Ulinzi nchini Marekani Pentagon imesema kuwa ndege za kijeshi pamoja na zile zisizokuwa na rubani ziliharibu magari saba ya kivita yanayotumiwa na wapiganaji wa Islamic State.
Imesema kuwa oparesheni hiyo ni ya kuwaunga mkono wanajeshi wa Iraq na wapiganaji wa kikurdi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni