.

Jumatatu, 11 Agosti 2014

Ruanda: Raia wa Ujerumani ashukiwa kuambukizwa Ebola


Kwa mara ya kwanza mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa hatari wa Ebola amegundulika nchini Rwanda na tayari amewekwa kwenye sehemu yake pekee huku uchunguzi wa madaktari ukiendelea kubaini ikiwa kweli ana ugonjwa wa ebola.
Mgonjwa huyo mwenye asili ya Ujerumani aliingia nchini Rwanda akitokea Liberia ambako ugonjwa huo sasa umekwisha gharimu maisha ya mamia ya watu.
Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwanidishi: Sylivanus Karemera
Mhairiri: Josephat Charo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni