.

Jumanne, 21 Oktoba 2014

SOMA ALICHOANDIKA WAKILI WA ZITTO KABWE KATIKA UKURASA WAKE WA FACEBOOK


Bw;  Msando   Albero   maarufu   kama  wakili  wa  Zitto   Kabwe

Ali Kiba; Diamond na Muziki:
Kila mwanadamu anapenda kufanikiwa katika jambo lolote analofanya. Mafanikio yanatokana na sababu nyingi lakini muhimu zaidi ni;
1. Kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
2. Kuona nafasi (opportunity) na kufanya maamuzi sahihi.
Diamond na Ali Kiba wote kwa pamoja wamefanya hayo yote na kufanikiwa. Ndio maana tunasikia kuhusu 'ugomvi' baina yao.
Binafsi niseme ni ugomvi wa kupikwa na hauna tija kwa muziki wa Tanzania. Na wale wote wanaofurahia au kushabikia hawana nia njema na ukuaji wa muziki wetu.
Ni mawazo ya kipuuzi kuamini kwamba Diamond atafanikiwa zaidi kama Ali Kiba hatafanikiwa. Au eti Ali Kiba atafanikiwa kama Diamond hatafanikiwa.
Tumefika mahali fikra zetu zimeganda. Hatutaki kushirikisha bongo zetu kuona mbali. Tabia hii iko kila mahali. Kwenye siasa, dini, michezo nk.
Kuna wanaoamini ili CCM ishinde lazima CHADEMA ife. Ili CHADEMA ishinde lazima CUF ife. Ili Yanga ishinde lazima Azam ife. Ili Ukristo ushinde lazima Uislamu ufe!!! NK
Na ni tabia hiyo hiyo wanaojiita TeamDiamond na TeamAliKiba wanaiendekeza. Hili ni la kukemea.
Kwa mtu yeyote anaependa maendeleo atakubaliana na mimi Diamond na Ali Kiba wote wanaweza kuwa maarufu na kupata mafanikio kwa PAMOJA na hakuna sababu ya mmoja kufeli ili mwingine afanikiwe.
Wote hawa wawili wana vipaji vya hali ya juu katika muziki. Wote wanao uwezo wa kuimba. Ila kila mmoja kwa aina yake.
Ushauri wangu kwa wote wawili ni kwamba nafasi ya mafanikio na umaarufu sio MOJA. Wala sio MBILI. Ni NYINGI sana. Hata wao wenyewe hawawezi kuzijaza. Kila mtu aendelee kufanya kazi kwa bidii na ubunifu.
Kwa Diamond niseme kwamba yaliyotokea Fiesta ni uonevu kwake. Lakini ni wakati yeye kuwa na busara na hekima na kuepusha mgogoro zaidi. Achukue kama changamoto katika kazi. Asiwape watu nafasi kutuharibia muziki na malengo ya kuukuza zaidi. Najua anaweza.
Kwa mashabiki tuhakikishe team zinabaki Liverpool na Real Madrid. Hizo teamDiamond na teamKiba zibaki kwenye kununua CD original, kuingia kwenye show, kuwapigia kura kwenye Awards, kuwashauri vizuri nk.
Ni jukumu letu kuutangaza muziki wetu kwa ulimwengu. Tutaweza tu endapo hatutawagawa wasanii wetu au kuwagombanisha.
"You don't become STRONG by making your fellow WEAK".
It is a false victory if you win a fight because your alleged opponent is weak. It is a true victory if you win a fight because you are strong.......
AGM

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni