.

Jumanne, 21 Oktoba 2014

Alichofanya T.I kabla ya kuondoka Tanzania kiko hapa >>>


Weekend iliyopita Dar es Salaam ilikua na ugeni wa wakali wa muziki kutoka kona mbalimbali za dunia ikiwemo Nigeria na Marekani.

Tamasha la Fiesta liliendelea kuchukua headlines na kuvunja rekodi kwa mahudhurio ya karibu watu elfu 50 ambao imefahamika walitoka hata kwenye nchi jirani ili kuja kumuona T.I. tu.


Stori za uhakika ambazo DStv imezipata ni kwamba T.I alitumia zaidi ya dola za kimarekani elfu 3 kufanya shopping dakika chache kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege Dar es Salaam kurudi kwao Atlanta Marekani.

Vitu alivyonunua ni pamoja na bendera ya Tanzania, ndala, mashati pamoja na vitu vingine vya asili ambavyo alivinunua kwa idadi kubwa kuashiria kuna watu aliwachukulia kama zawadi pia.


T.I alionekana kuifurahia Tanzania hata kwa kupost picha za Tanzania Instagram na kuweka caption ambayo ilikua inamshawishi yeyote kwamba Tanzania ni nchi nzuri.

Wanamuziki wengine waliocheza Fiesta, ambae ililetwa na Clouds FM, ni Ali Kiba, Diamond, Waje, Victoria Kimani, Ommy Dimpoz, Linah na Davido.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni