Matumizi hayo hatari ya Metakelfin yamegundulika
huku kukiwa na taarifa za maji ya betri za magari, kutumika kama
malighafi ya kutengeneza mkorogo unaotumiwa na baadhi ya wanawake
kuchubua ngozi zao.
Utafiti uliofanywa hivi karibuni na shirika lisilo
la kiserikali la Envirocare linalojihusisha na mpango wa kupunguza
madhara yatokanayo na bidhaa za vipodozi kwa binadamu na mazingira,
umebaini dawa ya malaria aina ya Metakelfin ni mojawapo ya kemikali
inayotumika kienyeji katika kutengeneza kipodozi cha kurembesha nywele.
Kwa mujibu wa mtafiti Issai Sen’genge, Metakelfin
ni miongoni mwa kemikali inayotumika kutengeneza mchanganyiko wa
kulainisha na kurefusha nywele.
Alisema idadi kubwa ya waliohojiwa, waliitaja dawa
hiyo ya malaria kuchanganywa ndani ya dawa nyingine za nywele ili
kupata mchanganyiko ambao husaidia kurembesha nywele.
“Swali lilikuwa kama kuna vitu vinavyotumika
katika kutengeneza mchanganyiko wa kupaka kwenye ngozi au nywele,
waliohojiwa walikiri kuchanganya, Metakelfin, Jik, maji ya betri na
kemikali nyingine,” anasema Seng’enge.
Kwa upande wake, Maria Kimiro ambaye ni mmiliki wa
saluni ya wanawake iliyopo Makongo jijini Dar es Salaam, alikiri
kusikia matumizi ya vidonge katika vipodozi lakini hana uhakika wa aina
ya dawa hizo.
“Nakumbuka kuna mtu nimeshawahi kumsikia
anazungumzia vidonge katika masuala ya vipodozi, lakini sina uhakika
kama ndiyo hiyo Metakelfin au vidonge vingine,”anasema Kimiro.
Asha Rashidi mkazi wa Tabata jijini Dar es salaam,
alikiri kuwa katika kutafuta urembo wanawake wanatumia vitu mbalimbali
hata vinavyohatarisha maisha ili mradi kutimiza azma yao.
Anasema kuwa hali hiyo mara kwa mara imekuwa
ikisababishwa na kuiga au kusikia kutoka kwa wengine bila kufikiria
madhara ya ambacho anatarajia kukifanya.
“Binafsi sijawahi kutumia hiyo Metakelfin kwa
kuwa nafahamu ni dawa ya malaria lakini naamini kuna watu ambao
wanaweza kuichakachua kwa namna wanavyoweza wakidhani kwamba inaweza
kuwa na matokeo mazuri kwenye ngozi au nywele,” alisema.
Wataalamu wa afya wanazungumziaje
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni