Na Mwandishi Wetu
BADO habari ya mjini ni skendo ya
kunaswa na madawa ya kulevya ‘unga’ inayomtafuna Video Queen wa Bongo,
Jacqueline Clifford Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ ambaye inadaiwa kuwa
mtandao wake wa biashara hiyo ni wa kutisha, Ijumaa limetonywa.
Habari kutoka kwa rafiki wa karibu wa
Jack ambaye aliomba chondechonde asitajwe, alidai kwa sasa vigogo
wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wamekuwa wakihaha kwa hofu kuwa
modo huyo anaweza kuwataja hivyo wanafanya kila linalowezekana ili
wamnusuru kama ilivyokuwa kwa Agnes Gerald ‘Masogange’.
Ilisemekana kuwa katika mtandao huo,
vigogo hao wenye maskani jijini Dar, Rwanda, Uganda, Kenya, Dubai,
Thailand, Italia na Hong Kong wamekuwa wakihaha kumuokoa Jack bila
mafanikio.
“Unajua China siyo rahisi kumchomoa kama
ilivyokuwa kwa Masogange (Agness Gerald) aliyenaswa Sauz (Afrika
Kusini) kwa sababu wale (China) Tanzania haikuwasaidia kupata uhuru kama
ilivyokuwa kwa Sauz.
“Ile ngoma ni mbichi, hakuna upenyo wa
rushwa pale. Ngojeni tusubiri hukumu maana itakuwa kali sana, nazijua
vizuri sheria za China juu ya madawa ya kulevya,” alisema rafiki huyo wa
Jack na kuongeza:
“Hakuna ishu iliyoniuma kama ya Jack kwa
mwaka uliomalizika.”
Katika nusanusa za gazeti hili, ilidaiwa
kuwa bosi aliyemtuma Jack ni mwanamke mmoja tajiri aishie jijini Dar
ambaye ana mtandao mkubwa wa biashara hiyo duniani.
Ili kuthibitisha kuwa mtandao uliodaiwa
kumtuma Jack unatisha na una watu wazito, ilielezwa kwamba mrembo huyo
hakuwa peke yake kwani alifuatana na warembo wawili, mmoja Mtanzania na
mwingine raia wa Rwanda ambao wao walifanikiwa kuwatoroka polisi wa
China.
Mbali na timu hiyo ya watu watatu
waliokuwa na mzigo mwilini, pia kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa
akiwasindikiza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni