Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana alitinga mahakama
kuu kupinga
kujadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya Chadema,Kikao ambacho kilikuwa
kikutane leo.
Hii ni kauli yake baada ya mahakama kumpa ushindi;
"Jana tulikwenda mahakamani kwa ajili ya jambo moja tu kutaka haki itendeke kwa sababu mahakaama ndiyo chombo cha juu kabisa kwenye nchi yetu cha kuweza kutenda haki mara baada ya kamati kuu ya chama changu kufanya maamuzi ya kunivua nafasi zangu ambayo niliandikiwa makosa 11
Hii ni kauli yake baada ya mahakama kumpa ushindi;
"Jana tulikwenda mahakamani kwa ajili ya jambo moja tu kutaka haki itendeke kwa sababu mahakaama ndiyo chombo cha juu kabisa kwenye nchi yetu cha kuweza kutenda haki mara baada ya kamati kuu ya chama changu kufanya maamuzi ya kunivua nafasi zangu ambayo niliandikiwa makosa 11
"Nilikata rufaa kwenye baraza kuu la chama ili baraza kuu liweze
kuona kama kamati kuu ilifuata taratibu za chama kufikia maamuzi yale
japo mimi naamini haijafuata taratibu za chama lakini kwa bahati mbaya
viongozi wangu wa chama changu wameamua kuendelea na kikao cha kamati
kuu.
"Hawajajibu barua yangu ya nia ya kukata rufaa na kuweza kupatiwa
taarifa na mwenendo wa kikao ili niweze kukata rufaa kwa mujibu wa
chama.
Kwa hiyo nimekwenda mahakani ili mahakama iweze kutoa maamuzi ya mimi
kuweza kupata nafasi ya kusikilizwa na kujadiliwa.
"Nashukuru Jaji John Utamwa ametoa amri ya muda ya kuzuia kamati
kuu
ya chama kunijadili mpaka hapo Chadema watakapoweza kujibu hoja
zilizotolewa na mwanasheria wangu Albert Msando.
"Leo tunarudi mahakamani kwa ajili ya kuendelea na kuweza kupokea
majibu kutoka Chadema lakini kikao cha leo kamati kuu imezuiliwa na
mahakama kujadili hoja yoyote inayonihusu,lakini pia mapingamizi yote
mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu aliyokua ameyaweka dhidi ya
mwanasheria wangu Jaji ameyatupilia mbali kwa hiyo kesi inaendelea.
"Muhimu katika hili ni haki na mimi kama mtu ambaye siku zote
natetea
haki sasa ni fursa yangu kutetea haki yangu mwenyewe ya kuweza
kusikilizwa ya kutumia taratibu zote za chama katika hali ya kawaida
baraza kuu la chama liitwe kwanza lijadili jambo hili kabla ya kikao
cha kamati kuu kuitwa".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni