.

Jumapili, 5 Januari 2014

WANGAPI TUNAWAJALI WAZAZI WETU WAKIWA KATIKA STAGE YA UZEE..? STORY HII NI FUNDISHO KWAKO


Mzee mmoja wamiaka 80 alikuwa kakaa na mwanawe wa kiume msomi mwenye umri wa miaka 45. Wakiwa wanaendela kuongea na mzee akimkumbusha mwanae mambo mazuri ya zamani mara jogoo akawika huko nje.
Mara yule babu akamuuliza mwanae, “ nini hicho kinapiga kelele mwanangu?”
Mtoto akajibu, “ Ni jogoo anawika huyo baba!!”
Mzee akatulia kama dakika kisha akauliza tena baada ya jogoo yule kuwika tena, “ Nini hicho kinapiga kelele mwanangu?”
Mtoto akajibu tena, “ Ni jogoo anawika huyo baba mbona husikii!!”
Wakaendela kuongea kwa dakika chache na kisha babu akauliza tena, “ ni nini hicho kilichokuwa kina piga kelele mwanangu?”
Kwa hasira mtoto akajibu, “ baba mbona unakuwa mgumu kuelewa ni jogoo huyo alikuwa anawika,sasa hujaelewa nini hapo baba????”
Mzee yule akauliza tena baada ya daikia moja, “mwanangu ni kelele za nini zilezilizosikika?”
Safari hii yule mtoto uvumilivu ulimshinda na kujibu kwa kelele na hasira, “ baba sipendi maswali yako ya kijinga, kwani hujui huyo ni jogooo, Au unataka tutafutane ubaya mida hii?????”
Taratibu babu yule alinyanyuka na kwenda ndani na kurudi akiwa kashika kitabu chake kidogo cha kumbukumbu alicho kiandika mika 42 iliyopita na kumpa mwanaye ambaye sasa ana miaka 45 ili akisome.
Mtotoyule aliumia sana baada ya kusoma maneno yaliyoandikwa miaka 42 iliyopita na baba yake wakati huo mtotohuyu alikuwa na miaka 3.Mtoto yule aliskia sauti ya jogoo aliwika na akamuuliza baba yake ile ni sauti ya nini…
Baba yake aliandika katika kumbukumbu zake , “Leo nina furaha sana kwani mwanangu kasikia sauti ya jogoo akiwika na kaniuliza mara 23 kuwa sauti ileni ya nini na wala sijachoka kumjibu na nikamkumbatia na kumwambia kila muda aniulize swali lolote nami nitamjibu kwani yeye ni furaha yangu”
Mtoto aliulizwa mara 4 tuu na baba yake lakini akaona ni kero na wakati baba aliulizwa mara 23 na bado akafurahi na kuona kapata bahati ya kuulizwa swali na mwanae.
Je ni wangapi leo ambao yunaona kero kupokea simu za wazazi wetu au hata kero kuwa nao karibu na hata kuwapa nafasi wao watuulize au kufurahi nasi hata mara moja tu????
Tunahitaji kubadili mienendo yetu na kuwafurahia wazazi wetu na kuona tuna bahati kuwa nao.Fikiri ni wangapi tunakosa bahati ya kuwa na wazazi wote wawili?

Kwanini Umpeleke Baba/mama/babu/bibi yako katika kituo cha kulelea wazeee? Je wewe ulivyokuwa mtoto hujiwezi wangekupeleka kituo cha kulea watoto ungejisikiaje sasa?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni