MWAKA ulianza vibaya kwa mke wa mtu ambaye jina
lake halikupatikana mara moja kumkimbia mumewe na kumfuata mume wa
msanii wa filamu, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ aitwaye Michael Sangu ‘Mike’
jambo lililosababisha ale kichapo cha nguvu na kuuanza mwaka mpya
vibaya.
Tukio hilo lililovuta hisia za wengi,
lilitokea siku ya mkesha wa mwaka mpya, usiku wa kuamkia Jumatano,
katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar ambapo Bendi ya African
Stars ‘Twanga Pepeta International’ ilikuwa ikikonga nyoyo za mashabiki
wake.
KAMERA ZA IJUMAA
Paparazi wetu aliyekuwa
ukumbini humo alimuona Mike akiwa upande mwingine na washikaji zake huku
wakiendelea kula raha wakati wa shangwe za mwaka mpya wakati mdada huyo
‘kibonge’ akiwa na mumewe na watu wengine wakifanya yao.
Ijumaa lilipata shaka
kidogo, baada ya kumuona dada huyo akimwacha mumewe kila wimbo
unapokolea na kwenda alipokuwa Mike kisha kucheza naye.
Harufu ya ugomvi ilianza kunukia mapema,
baada ya paparazi wetu kumshuhudia mume wa dada huyo akionekana
kumkaripia japo kwa sauti ndogo mkewe kila aporudi akitokea kucheza na
Mike.
ONYO HALIKUZAA MATUNDA
Pamoja na onyo
alilokuwa akitoa mume huyo kwa mkewe mara kwa mara, bado dada huyo
alionekana kumfuata Mike na kucheza naye tena kwa ukaribu kama vile
wanajuana.
Baadaye jamaa huyo aliamua kuwashirikisha marafiki
aliokuwa amekaa nao meza moja kuhusu tabia ya mkewe, wakamsihi asiende
tena kucheza lakini bado hakusikia.
“Sisi tulimwambia, mwenzako hataki
uende kucheza na yule msanii, anahisi labda kuna kitu kinaendelea lakini
hakusikia, sijui ni pombe zilimzidi au vipi,” alisema mmoja wa watu
waliokuwa wameketi meza moja na wanandoa hao muda mfupi baada ya tukio
la kichapo kutokea.
Akaongeza: “Kuna wakati alikuwa
akijifanya ameelewa, lakini sasa alikuwa akiaga na kujifanya anakwenda
msalani halafu mumewe akifuatilia anagundua kumbe amemfuata Mike ili
wacheze, jamaa akachukia sana.”
KICHAPO
Baada ya
mume kuona dharau za waziwazi zikifanywa na mkewe mbele ya watu aliokuwa
amekaa nao, aliamua kusimama na kumfuata alipokuwa akicheza na Mike.
Hakuwa
na haja ya kuuliza chochote, alimkamata mkewe na kuanza kumshushia
kichapo cha nguvu huku wengi wakiendelea kuponda raha kama vile hakuna
kilichotokea.
“Ni mke wake? Hizo ni dharau, acha
apigwe. Hawa wanawake wa Dar ni wajinga sana. Utamwachaje mumeo uende
kushobokea wasanii? Huu ni upuuzi. Ni haki ale kichapo,” alisikika
akisema jamaa mmoja aliyekuwa jirani na paparazi wetu.
DAMU CHAPACHAPA
Hasira
zilipompanda yule jamaa, hakuchagua mahali pa kupiga, alimvuta nywele
na kumpiga makonde kila sehemu ya mwili wake hali iliyosababisha damu
imwagike chapachapa (angalia picha ukurasa wa mbele).
Mashuhuda
walipoona damu imemwagika ndipo wakaingiwa na huruma na kuamulia ugomvi
huo.
UTETEZI WA MKE
Katika kujitetea, mwanamke
yule alimlaumu mumewe kwa kumpiga hadi kufikia kutoa damu kwa kosa la
kucheza na Mike akisema kwamba, haoni kosa lake.
“Mume wangu
unanionea tu bure, huyu sina uhusiano naye wowote ule... nacheza naye tu
kama marafiki. Simfahamu na wala sijawahi kumuona zaidi ya kwenye
filamu,” alisema mwanamke huyo.
MIKE HUYU HAPA
Kwa
upande wa Mike, alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu kisanga hicho
alisema, anamshangaa jamaa mwenye mke kwa sababu amemuonea mkewe bila
sababu ya msingi.
“Kuna kosa gani watu kucheza muziki? Hapa ni ukumbi wa muziki,
tena usiku. Hakuna mipaka, yeyote anaweza kucheza na yeyote. Ule mimi
naweza kusema ni ulimbukeni wa kutojua mambo.
“Amemuonea... yule dada
alikuwa anafurahi tu sherehe za mwaka mpya ambapo staili yake ya kucheza
labda imemkera mumewe lakini kama alikuwa hataki mkewe acheze na mtu
mwingine, si wangekaa tu chumbani kwao wawashe redio wacheze wawili tu
kuliko kuja kuleta kero kwenye kumbi za burudani?” alisema Mike.
Alipoulizwa
hajisikii vibaya kucheza na mke wa mtu alijibu kwa kifupi sana: “Kwanza
ningejuaje?”
MADAI MENGINE
Ndoa
ya Mike na Thea kwa sasa ipo kwenye mgogoro mzito ambapo wawili hao
wametengana huku sababu kubwa ikitajwa na vyanzo vyetu kuwa ni Thea
kumtuhumu mumewe kuwa hajatulia.
Bado tunafuatilia sakata hili,
likikamilika tutawaletea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni