Mwakilishi wa jimbo la Mwanakwerekwe Shamsi Vuai Nahodha amesena
anaungana na kundi la wazanzibar wanaotaka Zanzibar kuwa na mamlaka
kamili ndani ya katiba ijayo ya jamhuri ya muungano Tanzania.
Akizungumza na wanachama na viongozi katika ofisi za CCM mkoa wa
mjini kichama amesema katika baadhi ya maeneo ya kuendesha nchi suala la
mamlaka kamili ni muhimu kuimarisha uchumi wa Zanzibar.
Nahodha aliewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani na waziri wa ulinzi
na jeshi la kujenga taifa amedai yeye ni mtetezi wa suala la mafuta na
gesi liondolewe kwenye muungano.
Hata hivyo amesema anashangazwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya
siasa wanaodai sarafu ya Zanzibar, kiti cha umoja wa mataifa na wizara
ya ulinzi akidai masuala hayo yanahitaji gharama kubwa za uendeshaji.
Aidha Nahodha amesema wakati Zanzibar ikiendelea kuadhimisha miaka
50 ya Mapinduziu Zanzibar muungano utaendelea kubaki uti wa mgongo wa
maendeleo ya ulinzi na usalama wake.
Amesema licha ya mfumbo wa muungano wa serikali mbili kujaa matatizo,
lakini njia ya kuyapatia ufumbuzi ziko huru badala ya kun’gan’gania
muungano wa mkataba au serikali tatu akidai haiku salama na Zanzibar.Source: Mzalendo.net
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni