Boban atakatwa mshahara wake wa mwezi huu kwa kuwa hajaufanyia kazi yoyote tokea alipotakiwa kujiunga na wenzake tarehe 1 Desemba mwaka huu,mbali na Boban adhabu ya namna hiyo pia itamkuta kiungo Jerry Santo ambaye ni raia wa Kenya kutokana na kutotoa sababu zozote za kuchelewa kujiunga na wenzake kambini.
‘Ni bora tukapandisha vijana wetu wa U20 kwa kuwa tunajua watatusaidia na wana nidhamu ya hali ya juu kuliko hawa ambao ni wazoefu lakini wanatusumbua upande huo’.
‘Hatuwezi kumuongeza mkataba mtu ambaye tunaona kabisa nidhamu yake haituridhishi kama timu na hajatoa hata taarifa yoyote. Wa nini mtu kama huyo? Sisi tunaangalia maslahi ya timu ili ifanye vizuri’. .
Kwenye kumbukumbu Boban aliwahi kuondolewa kwenye kikosi cha timu ya Simba ambacho alikuwa amekitumikia kwa muda mrefu kutokana sababu za kiutovu wa nidhamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni