Amos Joseph enzi za uhai wake. |
Akisimulia mbele ya gazeti hili mkasa mzima, mtoa habari hii aliyetajwa kuwa dada wa marehemu anayejulikana kwa jina la Khadija, alisema siku ya tukio kaka yake aliamka asubuhi na kumuaga kuwa anakwenda bondeni kwa mkewe (Farida) kwa kuwa walikuwa nyumba tofauti.
Aliongeza kuwa, muda mfupi baada ya kaka yake kuondoka nyumbani hapo, wifi yake (Farida) alifika nyumbani hapo na kumwambia kuwa kaka yake ameumia sana aende akamuone.
Mtuhumumiwa wa mauaji, Farida.
“Mimi nilimshauri ampeleke hospitali tu nikidhani ameumia kidogo, kwa
sababu wamekuwa na kawaida ya kupigana mara kwa mara na tulishawaonya.
Wifi aliondoka na mimi nikaendelea na shughuli zangu.“Muda mfupi, uliingia ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi ukisomeka kuwa kaka yangu alikuwa amefariki dunia huku ujumbe huo ukinionya kutolia ili nisimshitue mama,” alisema Khadija.
Dada wa marehemu Amos.
Dada mwingine wa marehemu aliyejulikana kwa jila la Christina,
alisema yeye aliwahi kufika nyumbani kwa Farida na kumkuta kaka yake
akiwa amelala chali huku damu zikimvuja, muda mfupi polisi waliwasili na
kufanya taratibu zote muhimu.Marehemu Amoni alizikwa siku chache baada ya kufariki dunia kwenye makaburi ya Mburahati City jijini Dar huku Farida akiwa mikononi mwa polisi kwa upelelezi zaidi.
Dada wa marehemu.
Gazeti hili linaipa pole familia ya marehemu na linamuomba Mwenyezi Mungu ailaze pema roho ya marehemu Amosi-Amin.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni