Kupitia kipindi chake cha ‘In My Shoes’
cha jana, Wema Sepetu alieleza jinsi alivyojisikia baada ya baadhi ya
waigizaji wenzie wa Bongo Movie kugoma kuhudhuria msiba wa baba yake,
Balozi Isaac Abraham Sepetu, mwishoni mwa mwezi uliopita kwa madai kuwa
yeye hakuwa akifanya hivyo kwenye misiba mingine.
“Imeshatokea, wameacha kuja kwenye
msiba, ni wao,” alisema Wema. Sio Bongo movie nzima, ni baadhi tu ya
watu ambao wanauelewa na upeo mdogo ambao waliamua kutokuja. Lakini
niliona Bongo movie wengi, walikuwepo marafiki zangu wengi, akina
Batulli, akina Esha, Wolper alikuja, Lulu, JB alikuja, Jokate alikuja,
Adam Kuambiana alikuja. Ambaye napenda nimpe my special thanks and
appreciation, ambaye alijitolea from the beginning wa msiba mpaka to the
end ni Dokta Cheni kwakweli. Dr Cheni, I thank na ntazidi kumshukuru,”
alisema.
“Marafiki zangu kama akina Kajala, akina
Zamaradi, wale sio marafiki, wale tayari ni ndugu, kwahiyo siwezi
kuwaweka kwenye appreciation wala kwenye thanks.”
Katika kipindi hicho pia, Wema alisema
yeye na ndugu zake walijua kuwa baba yako ni muumini wa dhehebu la Roman
Catholic siku chache kabla ya kufariki dunia.
Balozi Issac Abraham Sepetu (71),
alizikwa kikristo katika kijiji cha Mbuzini,mkoa wa Kusini Unguja
October 30 ambapo mazishi yake yalihudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar,Dk
Ali Mohammed Shein pamoja na viongozi wengine.
Bongo5.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni