Jana uongozi wa klabu ya Simba ulitangaza kumsimamisha mwenyekiti wake Ismail Aden Rage.
Maamuzi hayo yalitokana na kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika hapo juzi,
Hizi ni Miongoni mwa sababu zilizotolewa kwenye mkutano wa waandishi wa habari zilizopelekea kusimamishwa kwa Mheshimiwa Rage.
Rage alisaini mkataba na Azam TV kwa ajili ya kipindi ya cha Simba TV bila kuishirikisha kamati ya utendaji.
Wakati Rage anasaini mkataba na Azam TV
tayari klabu ya Simba ilikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho
kuingia mkataba na kampuni ya ZUKU kwa ajili kipindi cha Simba TV
uliokuwa na thamani ya dola za kimarekani 300,000 kwa mwaka.
Kampuni ya ZUKU ilipokuwa kwenye
majadiliano na viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga jijini Nairobi,
kwenye mkutano huo Simba iliwakilishwa na Mjumbe wa kamati ya utendaji
Joseph Itang’are maarufu kama mzee Kinesi pamoja na mwanachama Evans
Aveva wakati Yanga iliwakilishwa na Makamu mwenyekiti Clement Sanga na
Francis Kifukwe,viongozi hao Simba Ghafla walisikia Rage kasaini mkataba
na Azam TV kwa ajili ya Simba TV.
Mheshimiwa Rage ndiye aliyesimamia
uhamisho wa mchezaji Okwi on CREDIT bila kuishirikisha kamati ya
utendaji,matokeo yake klabu hiyo mpaka leo imeshindwa kupata pesa ya
uhamisho wa mchezaji huyo.
.
Kutoitisha vikao vya kamati ya utendaji.
Sababu nyingine iliyoelezwa ni kitendo
chake cha kushindwa kuitisha vikao vya kamati ya utendaji, Kuendesha
klabu na kufanya maamuzi binafsi bila ya kushirikisha kamati hiyo ya
utendaji ambayo ilichaguliwa na wanachama
Hivi karibuni klabu ya Simba ilizindua
mchakato wa kutengeneza mpango mkakati (Strategic Plan) lakini cha
kushangaza mwenyekiti amekuwa hataki kuona mpango huo ukifanikiwa.
Kushindwa kuitisha mkutano wa
marekebisho ya katiba,kuchukua maamuzi binafsi ya kuhairisha mkutano
maalumu wa katiba uliotakiwa kufanyika Novemba, mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni