Mwanamziki aliyepata kutamba na Bendi ya FM Academia ya jijini Dar es Salaam, Rapa, Haristot Shungu ameuawa nchini China huku kifo chake kikitawaliwa na utata mkubwa.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichopo nchini China, rapa huyo
alikamatwa uwanja wa ndege baada ya kugundulika kuwa amebeba madawa ya
kulevya akiwa ameambatana na rapa mwingine wa Bendi ya Akudo Impact,
Kanal Top na wote wawili kuhifadhiwa mahabusu.
“Tulijua kama Haristot alikamatwa pamoja na Kanal Top lakini ghafla
juzi (Ijumaa) tukaambiwa kuwa amefariki dunia, hatujui kifo chake
kimesababishwa na nini lakini mwili wake unaonekana kama vile aliungua
na moto au mtu aliyechomwa sindano ya sumu,” kimesema chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi wetu aliwasiliana na Kiongozi wa FM
Academia, Nyoshi El Saadat na kumuuliza kama alikuwa na taarifa zaidi za
Haristot.
Nyoshi alikiri kuwa marehemu alikuwa mwanamuziki wao na kudai kwamba kifo chake kimetawaliwa na utata mkubwa.
“Haristot
alikuwa mwanamuziki wetu, mara ya mwisho aliaga kuwa anakwenda Ulaya
kwa mchumba wake, nimeshangaa kusikia ameuawa nchini China kiukweli
hakuna anayejua ukweli wa kifo chake,” alisema Nyoshi.
Credit: GPL
Credit: GPL
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni