Mchezaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry amepigwa picha akiwa amevalia jezi inayodhaniwa kuwa ndio jezi itakayotumiwa na klabu ya Arsenal kwa msimu ujao.
Jezi hiyo ina nembo ya wadhamini wapya wa Arsenal ambao ni kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Ujerumani ya Puma .
Puma walisaini mkataba mpya wa kuidhamini Arsenal kwa thamani ya paundi milioni 30 kwa mwaka ,udhamini ambao ulivunja rekodi ya mikataba yote ya udhamini nchini England .
Henry ni mmoja wa wachezaji bora wa miaka yote kwneye historia ya Arsenal na kuonekana kwake akiwa amevalia jezi hiyo kumefanya watu wengi kuamini kuwa huenda Arsenal wakawa tayari kuzindua jezi zitakazotumika msimu ujao.
Picha hiyo iliwekwa kwenye mtandao wa kijamii wa twitter kwenye akaunti ya mwanariadha wa England Linford Christie ambapo mwanariadha huyo anaonekana akiwa na Henry pamoja na wachezaji wa Arsenal Bacary Sagna na Olivier Giroud .
Mwanariadha huyo baada ya kugundua kuwa huenda akawa amevujisha siri ya jezi hiyo mapema kabla ya muda wake aliifuta picha hiyo muda mfupi baada ya watu kuanza kuizungumzia , hali iliyozidisha uvumi kuwa huenda jezi hiyo ikawa ndio jezi halisi itakayotumiwa na Arsenal.
Mtete Focus Blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni