Rais
wa Cameroon Paul Biya amemshawishi mshambuliajhi Samuel Eto'o kufikiria
kwa mara nyingine juu ya maamuzi yake ya kustaafu soka la kimataifa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya Chelsea
alikutana na wawakilishi wa Rais Biya jijini Yaounde wakijadili juu ya
hatima ya baadaye ya mshambuliaji huyo.
Baada ya kukutana hatimaye Eto'o, amekubali kurejea kuitumikia tena Cameroon.
Sasa anatarajiwa kusafiri kuelekea Ufaransa kujiunga na kikosi cha
timu hiyo ambacho kinajiandaa kwa ajili ya mchezo wa hatua ya mwisho
kusaka tiketi ya kufuzu kombe la dunia wakikabiliwa na mchezo dhidi ya
Tunisia.
Eto'o
mwenye umri wa miaka 32 hapo kabla aliwaambia wachezaji wenzake kuwa
hana nia ya kuendelea kuitumikia Cameroon kauli ambayo aliitoa baada ya
mchezo dhidi ya Libya ambao walishinda na kusonga mbele katika hatua ya
mwisho ya mtono.
Licha
ya taarifa za kujiondoa kikosini, bado kocha wa kikosi hicho Volker
Finke ameendelea kumtaja mchezaji huyo katika kikosi chake kitakacho
vaana na Tunisia kwani alikuwa bado hajawasilisha taarifa rasmi ya
tangazo lake hilo.
Eto'o amekuwa hana mahusinao mazuri na mamlaka ya soka ya nchi yake
tangu huko nyuma ambapo akiwa nahodha aliongoza mgomo wa kudai posho
kiasi hata kuvuruga mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria mwaka 2011.
Tukio hilo lilipelekea kufungiwa kwa michezo 15 kabla ya adhabu hiyo kupunguzwa na kuwa miezi minane.
Hii si mara ya kwanza kwa Rais Biya kukatisha majaribio ya kustaafu
kwa wachezaji, kwani aliwahi kufanya hivyo kwa Roger Milla ambaye
alirejea dimbani katika fainali za kombe la dunia mwaka 1990 nchini
Italia.
Mtete Focus Blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni