Shirika
la madaktari wasio na mipaka wanaotoa huduma za kitabibu nchini za
Afrika Magharibi dhidi ya Ebola limesema dunia inapaswa kuchukua hatua
za haraka kukabiliana na janga la ugonjwa huo.
Rais wa chama cha
madaktari wasio na mipaka Medecins sans Frontieres Joanne Liu amesema
anashindwa kuelewa kwamba ni kwanini ikiwa ni miezi saba sasa tangu
kulipuka kwa ugonjwa huo hadi ambapo hakuna hatua za haraka za kidunia
zilizochukuliwa hadi sana.Amelinganisha hatua za kimataifa zilizochukuliwa wakati wa janga la tetemeko la ardhi la Haiti mwaka 2010 kwamba makundi ya misaada ya kibinadamu yalikusanyika katika eneo hilo kwa lengo la kutoa misaada ndani ya saa 48 tu sasa iweje katika janga hilo ambalo limeshachukua muda mrefu.
Rais Joanne amsema idadi ya watalaam 300 waliowasili Liberia kutoka Marekani ni ndogo hali ambayo inaonyesha wazi kuhitaji kwa wataalamu zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni