Mike
Sonko ni yule Mwanasiasa mwenye vituko ambae alipata umaarufu sana toka
akiwa mbunge kwa kuwa na swagg zake kivyakevyake, alikua mbunge kijana
ambae anaingia na hereni bungeni, blingbling kibao kama cheni na pete
kama anavyoonekana ametupia kwenye hii picha hapa juu akiwa sasa ni
Seneta wa jiji la Nairobi.
Sasa juzi kati Rais Uhuru Kenyatta alikwenda The Hague Uholanzi
kwenye Mahakama ya ICC kwa hiyo Wakenya wenzake wanaopinga huo uamuzi wa
ICC na kuona ni usumbufu wakajilipia nauli zao ili kwenda kumsupport
ambapo Seneta huyu ni mmoja wa waliojilipia na kulipia wengine pia.
Pamoja na Sonko kwenda huko akiwa na dukuduku la kukerwa na maamuzi
ya Mahakama hiyo akiitaka imuache Rais wao wa Kenya afanye kazi, aliamua
kuvaa tshirt yenye maandishi ya Kiswahili ‘ikiwatusi’ Wazungu kama
anavyoonekana kwenye hii picha hapa chini.
Kwenye hizi picha hapa chini anaonekana Seneta wa jiji la Nairobi
Mike Sonko na Tshirt ambayo alianza kuivaa toka akiwa Airport Kenya
kwenda Uholanzi yenye maneno yanayosomeka >>> ‘mumheshimu Rais wetu takataka nyinyi gasia‘
Kwenye
picha nyingine Sonko anaonekana akiwa amewasili mahakamani ICC na
kikosi chake kisha wakafanya maandamano mafupi kabla ya kumpa support
Rais Uhuru kwa kuimba wimbo wa taifa na nyimbo za kizalendo wakati kesi
ya Uhuru ikiwa inaendelea Mahakamani.
Tayari Rais Uhuru Kenyatta amerejea Kenya jana asubuhi na kupokewa na
maelfu ya Wakenya ambao hawakupendezwa na kilichofanywa na Mahakama
hiyo.
Muda mfupi tu baada ya kuwasili jana Rais Kenyatta alipiga vijembe Mahakama hiyo kwa kusema ‘Walikua
wanafikiria kwamba tutakataa kwenda mi nikawaambiwa ile kitu itakataa
kuja huko ni Urais wa Wakenya, tumeenda tumekaa huko masaa matatu
hatujaambiwa chochote… hatukufungua mdomo sasa hata nashindwa kujua
nilikwenda kufanya nini‘
‘Ile kitu hawajafahamu kwa vichwa vyao
ni kwamba kama nchi ya Kenya tumetoka safari ndefu, na wasifikiri ya
kwamba hatujui ni mahali gani tulifanya makosa, sisi tunawaambia
hapana….. tuko na suluhu ya shida zetu‘ – Uhuru
Unaweza kusikiliza hii stori zaidi kwa kubonyeza play hapa chini…
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni