Shirika
la madaktari wasio na mipaka wanaotoa huduma za kitabibu nchini za
Afrika Magharibi dhidi ya Ebola limesema dunia inapaswa kuchukua hatua
za haraka kukabiliana na janga la ugonjwa huo.
Rais wa chama cha
madaktari wasio na mipaka Medecins sans Frontieres Joanne Liu amesema
anashindwa kuelewa kwamba ni kwanini ikiwa ni miezi saba sasa tangu
kulipuka kwa ugonjwa huo hadi ambapo hakuna hatua za haraka za kidunia
zilizochukuliwa hadi sana.
Amelinganisha hatua za kimataifa
zilizochukuliwa wakati wa janga la tetemeko la ardhi la Haiti mwaka
2010 kwamba makundi ya misaada ya kibinadamu yalikusanyika katika eneo
hilo kwa lengo la kutoa misaada ndani ya saa 48 tu sasa iweje katika
janga hilo ambalo limeshachukua muda mrefu.
Rais Joanne amsema
idadi ya watalaam 300 waliowasili Liberia kutoka Marekani ni ndogo hali
ambayo inaonyesha wazi kuhitaji kwa wataalamu zaidi.
Kinshasa mwaka 1955, janga la HIV lilikuwa linatesa mjini humu na kote nchini DRC hasa mkoa wa Katanga
Ugonjwa wa ukimwi uligunduliwa miaka ya 1920 mjini Kinshasa, nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo. Wanasayansi wameeleza.
Wanasayansi
wa kimataifa wanasema ongezeko la watu,vitendo vya kukutana kimwili na
shughuli za usafirishaji kwa njia ya reli zilifanya virusi vya ukimwi
kuenea.
Ripoti inasema kuwa biashara ya ngono, ongezeko kubwa la
watu na vitu vyenye ncha kali kama sindano kwenye zahanati huenda
kulichangia kusambaa kwa ugonjwa huo DRC.
Wakati huo huo reli
ilikuwa ina watu takriban milioni moja waliokuwa wakiingia na kutoka kwa
wingi jijini Kinshasa kwa mwaka,wakisambaza virusi kwenda kwenye miji
mingine.
Takriban watu milioni moja walikua wakitumia reli ya Kinshasa mwishoni mwa mwaka 1940.
Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga.
Inaarifiwa virusi vya HIV ni sawa na virusi vya Sinium vinavyopatikana katika Sokwe
Ukimwi ulitambulika kuwa janga kimataifa mwaka 1980 na uliathiri takriban watu milioni 75.
Ugonjwa huu una historia ndefu barani Afrika , lakini ulipotokea ugonjwa huu bado ni mjadala mrefu.
Timu
ya wanasayansi kutoka chuo cha Oxford na chuo cha Leuven, nchini
ubelgiji walitafiti chanzo cha ugonjwa wa ukimwi wakisema kuwa ulianzia
kwa Sokwe.
Virusi vya HIV ni sawa na virusi vinavyopatikana kwa
Sokwe ambavyo vinajulilkana kama Simian ambavyo vinadhaniwa vilitoka kwa
Sokwe na kuambukizwa binadamu kupitia kwa damu wakati wakitafuta nyama
ya wanyamapori.
Virusi hivyo vilikuwa na muundo tofauti na muundo
huo ulikuwa unabadilika kila wakati. Virusi vya kwanza viliwaathiri
maelfu ya watu nchini Cameroon.
Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga.
Vurusi vya HIV
Idadi kubwa ya wanaume
waliokuwa wanafanya kazi mijini na idadi ya wanaume ndio ilikuwa kubwa
kuliko wanawake na hivyo biashara ya ngono ikawa kubwa sana.
Mmoja
wa watafiti Profesa Pybus anasema kuwa mambo mawili yanesaidia
kupunguza maambukizi. Kwanza hamasisho la serikali kuwatibu wagonjwa kwa
maradhi tegemezi.
Jambo la pili ingekuwa mfumo wa usafiri ambao
uliwawezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine huku ugonjwa
ukienezwa zaidi.
Takriban watu milioni moja walikua wakitumia reli ya Kinshasa mwishoni mwa mwaka 1940.
Virusi
vielendelera kuenezwa kwa nchi jirani ya Brazzaville na mkoa wenye
madini wa Katanga ambao ulikuwa kitovu cha ugonjwa huo.
Virusi havikukomea tu nchini Congo bali vilianza kuenezwa kote duniani
Mgonjwa
wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola amegundulika nchini
Marekani, imethibitishwa katika mji wa Dallas, Texas.
Maafisa
katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian
wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo.
Mgonjwa
huyo anasemekana kuwa ni mtu anayeaminika kuambukizwa ugonjwa huo
nchini Liberia kabla ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo.
Zaidi ya
watu 3,000 tayari wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola huko
Afrika Magharibi na idadi ndogo ya wafanyakazi wa Marekani wa mashirika
ya misaada wamepata nafuu baada ya kupelekwa kutibiwa Marekani.
Jumatatu,
maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya
Dallas wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa
virusi vya Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo.
Shirika la
Afya Duniani, WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000 wamekufa
kutokana na virusi vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka Liberia.
Nchini
Nigeria, nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kuna wagonjwa 19
waliothibitika kuugua ugonjwa wa Ebola na watu wanane wamekufa tangu
mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa nchini humo mwezi Julai..
Kuna mgonjwa mmoja aliyethibitika nchini Senegal, lakini hakuna taarifa za kifo mpaka sasa.
Ebola ni ugonjwa hatari wa virusi kuwahi kuzuka duniani.