.

Jumanne, 7 Oktoba 2014

APELEKWA HOSPITALI BAADA 'MASHINE' KUSIMAMA KWA SAA 17




 Mfanyakazi mmoja wa hoteli nchini Uingereza alilazimika kutoa painti mbili za damu (Takriban lita moja) kutoka kwenye uume wake- baada ya kusimama kwa muda wa saa 17 mfululizo.
Madaktari kwanza walijaribu kupunguza kasi ya damu kwa kijana huyo, Jason Garnett, kwa kupiga sindano 24 moja kwa moka kwenye nyeti zake.
Tovuti ya Metro imesema 'mashine' ilisimama kuanzia siku ya Ijumaa asubuhi alipoamka. Kijana huyo, 23, alijaribu kila aina ya njia, ikiwemo kukimbia, na kuoga maji ya baridi sana, kabla ya kupelekwa hospitali na rafiki yake.
Hospitali iligundua kuwa Garnett alikuwa na maradhi ambayo ni haba kuonekana yajulikanayo kama priapism - ambapo uume husimama bila kukoma. Maradhi hayo hayasababishwi na hamu ya kutaka kufanya mapenzi, lakini iwapo mtu hatopata tiba, inaweza kuharibu uume, imeripoti tovuti ya News.com.au.
Akizungumza na gazeti la The Sun, amesema: "Yaani kuishia hospitali na jambo hili, ni moja ya siku ya aibu zaidi kwangu duniani.
"Kuona wakichoma sindano 'mashine' yangu ilikuwa jambo gumu sana kwangu- kama kutazama filamu ya kutisha. Maumivu yalikuwa asilimia 100."
Amesema baada ya sakata hilo, nyeti yake ina majeraha 'kibao'.
Picha: © Getty Images / Peter Dazeley

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni