Mwanamke
wa kwanza kushika wadhifa wa urais nchini Brazil 2011, Diana Rousseff
amechaguliwa tena kushika wadhifa huo katika uchaguzi mkuu uliofanyika
siku ya Jumapili Oktoba 25 nchini humo.
Baada ya kutangazwa kushinda katika kinyang’anyiro hicho, Rousseff
mwenye umri wa miaka 66 amesema anahitaji kufanya vizuri katika awamu
hii ya uongozi wake huku akisifia jitihada zake na rais aliyemtangulia
Luiz Inacaio Da Silva kuwa katika vipindi vyao vya uongozi wametatua
tatizo la ajira kwa kiasi kikubwa.
Rousseff ameshinda kwa 51.59% ambapo mpinzani wake Aecio Neves amepata kura 48.41%.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni