.

Alhamisi, 2 Oktoba 2014

Mgao wa Umeme kubaki histori Tanzania 2015




Tatizo la mgao wa  umeme nchini linatarajiwa kwisha ifikapo mwezi   machi  mwaka  2015.
Hatua hiyo itafikiwa kutokana na mtambo unaojengwa katika kituo kingine cha umeme kilichopo  Tabata kinyerezi  kuongezeka  na   kitakuwa  na uwezo wa kuzalisha umeme  mega watts 150.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi amesema    hadi sasa wana jumla ya vituo kumi ambavyo  vinazalisha  umeme.
Naye Mkuu wa Mkoa Said Mecky Sadick ametoa wito kwa wanachi kutunza miundombinu  ili kusudio lililowekwa katika maendeleo ya nchi hususan katika gesi na umeme liweze   kufikiwa kwa wakati.
Serikali imeweza kugharimia mtambo wa umeme katika kituo hicho kilichopo Tabata kinyerezi kwa Dollar million 139 ambazo ni fedha   za serikari   na sio za   ufadhili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni