.

Jumanne, 31 Desemba 2013

HAYA NDO MATUKIO YALIYOSISIMUA 2013 ..... KUWAHUSU DIAMOND, WEMA, MANDELA NA WENGINE WENGI

hizi mtu tatu ziwache 
Tanzania ilizizima ulikuwa ni msiba mkubwa sana
RIP Ngweah
Bosslady wa Tanzania kukamatwa
na sembe Macau
kila mtu anasema lake
FineAssGirl kukamatwa na sembe SA
na kwakipindi kifupi kuachiwa
huru na kurudi home salama salmin
wengi limewakera ila wamesema hewala

Tukiwa tumebakiza saa chache kabla hatujaingia mwaka mpya kwanza kabisa tumawashukuru wadauzii kwa kuwa pamoja na sisi mwaka mzima, senkyuuu
kwa upande wangu haya ndio matukio yaliyonisisimua mwaka 2013 kama una yako usisite ktk comment jimwageee umwagie ilimradi usitukane matusi maana huu mwaka una miezi 12 kama mingine ila ulikuwa mrefu matukio lukuki.....
leo tunakumbushana vitu vilivyo hit ndani na nje ya Tanzania
ninakutakia kila la kheri na mwaka mpya na jipange mapema hakuna lisilowezekana chini ya juu, ni kumomba Mungu tuu
senkyu 
cdt, The Choice

CCM Kigoma wampigia 'debe' Zitto CHADEMA..!!


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kigoma Mjini kimeunga mkono hatua ya Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA aliyevuliwa madaraka, Zitto Kabwe kusimamia demokrasia na matumizi sahihi ya fedha katika chama chake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Kwa Noti Ujiji Mjini Kigoma, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kirumbe Ng’enda alisema kuwa Zitto alikuwa sahihi katika kusimamia mambo hayo makubwa mawili.
Alisema kuwa CHADEMA kama chama ambacho kinajinasibu kusimamia demokrasia nchini kilipaswa kuonesha kwa vitendo utekelezaji wa jambo hilo, lakini badala yake baadhi ya viongozi wa chama hicho wameonesha kuwa chama hicho hakitekelezi demokrasia.
Ng’enda aliongeza kuwa kitendo cha kutangaza kuwa na nia ya kuwania uenyekiti kwa Zitto imekuwa tatizo kubwa kwa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, hali ambayo uongozi wa CHADEMA umeona ni uhaini na kuamua kumvua madaraka.
Aidha akizungumzia matumizi na usimamizi wa fedha za ruzuku ambazo vyama vya siasa vinapewa Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya CCM alisema kuwa hilo ni suala la kisheria na ni lazima kila chama kioneshe matumizi sahihi ya fedha hizo kwa kuwa na taarifa ya mahesabu iliyokaguliwa ambapo Zitto kama Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali analo jukumu la kusimamia na kuwasilisha bungeni taarifa hizo.
CHADEMA wanashangaza sana badala ya kuonesha taarifa iliyokaguliwa wanaanza kumsulubu Zitto kwamba anawasaliti, mara anatumiwa na CCM kuwahujumu, yote hiyo inaonesha hakuna demokrasia wala utawala bora kwa viongozi wa chama hicho,” alisema Kirumbe Ng’enda.
Awali akizungumza katika mkutano huo Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Kigoma Mjini, Zuberi Mabie alisema kuwa CHADEMA imeonesha haina ukomavu wa kisiasa wala utawala wa pamoja na ndiyo maana baadhi ya viongozi kwa kuona kama chama ni mali yao hawataki kukosolewa.
Mabie alisema kuwa kukosolewa kwa viongozi ni jambo la kawaida na kwamba CHADEMA inakosea kwa kiasi kikubwa kumsulubu Zitto ambaye ameonyesha msimamo na uzalendo wake kwa Taifa badala ya chama kwa kusimamia utekelezaji wa sheria na katiba ya nchi.

Picha ya Waheshimiwa Sugu na Mwesigwa wakicheza 'Ndombolo'


 Waheshimiwa Sugu na Mwesigwa

Picha za mwanaume aliyepanda juu ya mnara wa simu jijini Dar na kugoma kushuka mpaka Rais Kikwete aje asikilize kero zake



Mwanaume mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja amepanda juu ya mnara wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom uliopo Ubungo katika eneo la ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  jijini Dar es Salaam na kutaka kujirusha.
 
Mwanaume huyo amedai alitaka kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kudai kufungwa miaka sita jela kwa kubambikiziwa kesi na  polisi.
 
Mwanzoni alikataa katakata kushuka kutoka katika mnara huo akidai mpaka Rais Kikwete afike eneo hilo aweze kumweleza kero yake hiyo japo wanausalama walifanikiwa kutumia mbinu zao kumshawishi asijirushe na kufanikiwa kushuka naye.
 
 
 
Jamaa huyo akiwatuhumu polisi kwa kuwabambikiza kesi wananchi wakati akiongea na wanahabari baada ya kushushwa kutoka kwenye mnara.

JACK PATRICK MATESO SAA 48, DADA YAKE AMLILIA, ASEMA ALIMUONYA

Stori:  Jelard Lucas
HABARI ya kufungia mwaka 2013 na kufungua pazia la mwaka mpya wa 2014 ni madai ya mwanamitindo kiwango Bongo, Jacqueline Patrick kukamatwa katika  Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akiwa na mzigo wa madawa ya kulevya aina ya heroin lakini Risasi Mchanganyiko linaangaza mapya zaidi juu ya sakata hilo.

Macho na masikio ya Wabongo wengi kwa sasa ni juu ya mwenendo wa madai hayo, wakati gazeti hili likiendelea kupekenyua limenasa mpya kuwa, Jack yupo kwenye mateso makali kutoka kwa askari wapelelezi nchini humo wanaotaka kujua mtandao unaomuunganisha katika mchezo huo.

SAUTI KUTOKA CHINA
Chanzo chetu makini kilichopo China ambacho kinapiga kitabu kilieleza kuwa, katika kufuatilia ishu hiyo, juzi Jumatatu, Desemba 30, 2013, alikutana na kizingiti cha kushindwa kuonana na Jack katika mahabusu aliyowekwa kwa maelezo kwamba, uchunguzi bado unaendelea.

Raia huyo wa Tanzania aliyedai ana ukaribu na Jack, kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini, alisema mengi kuhusiana na mateso anayopata mrembo huyo hivi sasa.
“Ni kweli Jack amekamatwa hapa Macau. Hilo halina ubishi kabisa. Sheria za huku zinatofautiana kati ya jimbo na jimbo. Nilifika mahabusu aliko kwa lengo la kutaka kumwona lakini nilikataliwa. Nimeambiwa hawezi kuonana na mtu yeyote hadi Machi, mwakani (mwaka huu). Bado wanaendelea na uchunguzi kwanza.

“Unajua wanajaribu kufichaficha mambo ili polisi waweze kufanya upelelezi wao vizuri lakini nimepenyezewa taarifa kuwa ataingizwa chumba cha mateso ili abanwe na kutaja mtandao wake. Wanajua yeye wameshamkamata, lakini wanataka kufahamu mzigo alitumwa na nani, ameutoa nchi gani na unakwenda nchi gani?

“Lengo la kufanya hivyo ni kukomesha mtandao mzima wa madawa ya kulevya. Si ajabu akawa kwenye mateso kwa kipindi chote hicho kama hatakuwa mkweli lakini kwa sasa ataingizwa kwenye kikosi cha kwanza.

“Hapo atakalishwa kwenye chumba cha mateso kwa siku mbili mfululizo (akimaanisha saa 48). Ni mateso makali sana. Wataalam wanajua wanafanyaje ili mtuhumiwa aweze kuzungumza ukweli kwa muda mfupi. Sasa hapo ikishindikana ndipo anaweza kuhamishiwa kwenye kikosi kingine,” alipasha mtoa habari wetu na kuongeza:

“Ni kama huko Bongo tu. Unaposikia chumba cha mateso ya wapelelezi maana yake shughuli yake siyo ndogo. Mimi namuonea huruma sana Jack, lakini najiuliza, hivi ni kwa nini huwa hawajifunzi kupitia wenzao?

“Si juzi tu wengine (Agnes Gerald ‘Masogange’ na Melisa Edward) wamekamatwa kwa madawa hayohayo na walisota kwa muda mrefu? Kwa nini hawasikii jamani? Namuhurumia sana kwakweli.”

KUMBE DADA YAKE ALIMUONYA
Habari kutoka kwa mtu wa karibu na dada wa Jack zinasema kuwa, wakati akitaka kusafiri akitokea Bongo, alimweleza dada yake juu ya mpango wake huo, akamuonya lakini modo huyo alikataa.

“Alimfuata dada yake na kumweleza mchongo mzima kuwa alitaka kwenda na mzigo China, dada yake akamwambia aachane na hizo biashara, akakataa. Jack alifikia hatua akamwambia dada yake kuwa hana mtoto, hana mume wala ndugu anayemtegea kwa hiyo yupo tayari kwa lolote kwani hakuwa na cha kupoteza.

“Kama angemsikiliza dada yake (jina linahifadhiwa) haya yote yasingemkuta na asingeingia kwenye mateso ya namna hii,” alisema mtoa habari wetu huku akiendelea kusisitiza jina lake lisionekane mahali popote kwenye ukurasa huu.

ABEBESHWA MZIGO, ALIPWA MALIPO YA AWALI
Ilizidi kusemekana kuwa, alipokaribia kuondoka Bongo, Jack alimwambia dada yake kwamba anakwenda kambini (kituo cha kuingiza mzigo tumboni) ambapo aliporejea kwa dada’ake alimuonesha dola za Kimarekani 21,000 (zaidi ya shilingi milioni 33) ambazo ni malipo ya awali huku akimwambia alishabebeshwa nusu ya mzigo.

Hata hivyo, habari zinasema Jack alimwambia dada yake huyo kuwa hakuwa akijisikia kusafiri lakini kwa kuwa anatafuta maisha aliamua kuondoka baada ya mzigo kukamilika wote siku iliyofuata.

INA MAANISHA NINI?
Kwa mujibu wa maelezo hayo, Jack aliondoka na unga hapahapa Bongo kwenda Thailand kupitia Nairobi, Kenya na baadaye Macau, China ambako alinaswa.

MASTAA WAFUNGUKA
Watu wamekuwa na mitazamo tofauti kulingana na ishu hiyo lakini Risasi Mchanganyiko lilipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya mastaa wa Bongo ambao wameeleza maoni yao kuhusiana na sakata hilo la Jack.

Katika mahojiano na waandishi wetu, tulitaka kusikia kutoka kwao namna wanavyolinganisha tabia ya kujihusisha na biashara za kusafirisha madawa ya kulevya na vitendo vya umalaya ambapo wametoa maoni tofauti.

JACQUELINE WOLPER:
“Mh! Mwenzangu, bora uwe na mabuzi (wanaume wenye mkwanja) 40 kuliko kufanya biashara ya madawa ya kulevya. Nawaomba mastaa wenzangu wasikubali kubebeshwa madawa kwa kudanganywa eti na dola 30,000, kamwe haiwezi kubadili mfumo wa maisha yako.” 

REHEMA CHALAMILA ‘RAY C’:
 “Madawa ya kulevya hayakubaliki, yalinitenda sana haya madude! Kabisa tulinde vizazi vijavyo kwa kupiga vita madawa ya kulevya. Fanya yote lakini siyo madawa ya kulevya.”

SHAMSA FORD:
 “Nasema hivi, bora umalaya japo pia si mzuri kuliko kudili na biashara ya madawa ya kulevya. Nawaomba waachane na vitu hivyo kwani vinatumaliza kisanii... lakini nasisitiza kutulia na bwana mmoja ni vizuri sana kuliko kurukaruka.”

JOKATE MWEGELO:
 “Hakuna aliye mkamilifu lakini kama kitu ni kiovu ni kiovu tu hata kama mimi na wewe tunakifanya, kimsingi hakuna bora na anayesema kuna ubora basi hajitambui. Vyote vinadhalilisha utu na thamani ya mwanamke. Mwili si wa kuchezewa.”

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’:
“Tukitumia majina yetu vizuri, hakuna atakayejihusisha na yote hayo... tujitume kufanya kazi, umalaya unaweza kuwa bora kuliko kufanya biashara ya madawa ya kulevya kama utabanwa kuchagua maovu hayo. Maisha ya Ughaibuni yatatumaliza kwani tunaiga kwa kukurupuka bila kuelewa.”

TUMETOKEA HAPA
Jack anatuhumiwa kukamatwa na madawa ya kulevya Desemba 19, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Macau, China akitokea jijini Bangkok, Thailand akiwa safarini kwenda Guangzhou nchini China.
Ilielezwa kuwa unga aliokutwa nao una uzito wa kilo 1.1  ndani ya kete 57 huku thamani yake ikitajwa kuwa ni  zaidi ya shilingi milioni 223.
Bado yupo mikononi mwa polisi wa China wakati upelelezi wa awali ukiendelea ambao utafikia tamati Machi, mwaka huu kabla ya kuingia hatua inayofuata.
-GPL

Unatamani kuona Magazeti ya Tz yameandika nini kwenye siku hii ya kwanza ya 2014?


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.



Jumatatu, 30 Desemba 2013

Hatimaye Rasimu ya Katiba Mpya yapendekeza Muungano wa Serikali tatu...!!


Rasimu ya Katiba hii ni ndefu kuliko ya kwanza in ibara 271 ya kwanza ilikuwa na ibara 240 .Wananchi wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala bora  kama  ifuatavyo:

1-lugha ya kiswahili ni lugha ya taifa.

2-Madaraka ya Rais yamepunguzwa.
3-wabunge wasiwe mawaziri
4-kuwe na ukomo wa wabunge
5-wananchi wawajibishe wabunge
6-spika/naibu wasiwe wabunge wala viongozi wa juu wa vyama vya siasa.

7-kuwepo na jeshi moja la Polisi na Usalama wa Taifa.

MUUNGANO
Muungano umependekezwa uwe wa serikali tatu kutokana  na  kero  mbalimbali  zilizoko pande zote mbili. Baadhi ya kero hizo ni kama ifuatavyo:

 
Kero za wazanzibar
1-Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Tanzania na hivyo kutumia mwanya huo kujipatia misaada toka nje
2-mambo ya muungano yamekuwa yakiongezeka
3-kumuondoa rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais

Kero za  Tanzania Bara.

1-Zanzibar imebadili katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamuhuri ya Muungano
2-Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar  wakati wazanzibar huku Tanganyika wanaruhusiwa


Mambo mengi ya Muungano yamebadilishwa bila kufuata Katiba. HIVYO:
 

** TUME imependekeza  muundo wa muungano uwe  wa  serikali 3.

Hii ndo Rasimu ya Pili ya Katiba mpya iliyokabidhiwa kwa Rais Kikwete leo...Pata fusa ya Kuisoma haapa...!!


Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete (kulia) Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya leo.
 ** Hii  ndo  Rasimu  ya  Pili  ya  Katiba  mpya  iliyokabidhiwa  kwa  Rais  Kikwete  leo...Nimejitahidi  kuikuza  ili  iweze  kusomeka  vizuri....



Rasimu  hii  ni  ndefu  kidogo, ina  ibara  271  ikilinganishwa  na  ile  ya  kwanza  ambayo  ilikuwa  na  ibara  240...



Rasimu  iko  hapo  chini, ukipabofya  itafunguka  kwenye  tab  mpya  ili  uweze  kuisoma  vizuri....Upande  wa  juu  kushoto  kuna  option  ya  kui download....
<< RASIMU YA  PILI, BOFYA  HAPA>>
Bofya  hapo  juu  uisome  rasimu  ya  pili  ya  katiba

HUYU NDIO ALIYE CHAGULIWA NA RAISI KUWA MKUU WA JESHI LA POLISI BAADA YA IGP MWEMA KUSTAAFU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence) katika Jeshi hilo la Polisi.
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations). Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne,  Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam

MTANZANIA HUYU KATAJWA KUWA NI MOJA YA WANAWAKE WAREMBO ZAIDI BARANI AFRIKA..!!

Millen_Magese-31
Jarida la Glitz Africa limetoa orodha ya wasichana 20 warembo zaidi barani Afrika (20 Most Beautiful Women in Africa) ambapo hata hivyo imetawaliwa na wanawake wa Nigeria na Ghana.
Millen-Magese-x-Joice-Jacobs_1-2
Ni Happiness Millen Magese pekee amekuwa mwanamke kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kuingia kwenye orodha hiyo.
Millen_Magese-31
Orodha nzima ni hii:
Leila Lopes (Angola), Vimbai Mutinhiri (Zimbabwe), Oluchi Orlandi (Nigeria), Yvonne Nelson (Ghana), Dillish Mathews (Namibia), Agbani Darego (Nigeria), Tiwa Savage (Nigeria), Stephanie Linus (Nigeria), Genevieve Nnaji (Nigeria), Joselyn Dumas (Ghana), Yvonne Okoro (Ghana), Jackie Appiah (Ghana), Millen Magese (Tanzania), Omotola. Jalade-Ekeinde (Nigeria), Zainab Sheriff (Sierra Leone), Naa Okailey Shooter (Ghana), Nadia Buari (Ghana), Lerato “Lira” Molapo (South Africa), Babalwa “Barbz” Mneno (South Africa), Elham Wagdi (Egypt).