Wengi
wa wananchi wamekuwa wakilalamika sana kuhusu mwenendo wa Bunge la
Katiba kuendelea ili hali ukweli ni kuwa kundi la wanaotetea maslahi
halisi ya Wananchi (UKAWA) hawapo na pia mwenendo wa kuwatisha wanaotoa
elimu na maudhui ya Rasimu ya 2 ya Katiba, kupitia vyombo vya Habari na
midahalo, ufahamu ambao ni haki ya kila raia.
Mitaani,
watu wengi wanakasirika pia kuwa Taasisi ya kutetea haki za Binadamu
(TLHRC) na Jukwaa la Katiba (JUKATA) kuendelea kutokuchukua hatua za
kusheria, ambavyo wanasema ni ishara mbaya na kuwa wanaachia watawala
waendelee kufanya wapendavyo kuunda katiba yao kwa kupitia wingi wao na
kwa kumtumia Spika ambaye ameshindwa kuwa na dira ya kitaifa.
Wengi
wanatoa maneno ya hasira wakisema kuwa …”kama Legal and Human Rights
Centre (LHRC) mnao uchungu halisia kama tujuavyo, na jinsi
walivyoonyesha wajumbe wenyewe wa Tume ya Warioba, tunaomba pamoja na
timu ya JUKATA mpeleke ‘zuio’ mahakamani kuhakikisha kama yafaa Mahakama
ilazimishe yafuatayo ili kufanya Bunge la Katiba lizingatie maslahi
mapana ya utaifa na sio vikundi:
Kuamuru
Bunge la Katiba Kusitishwa kwa muda ili kuruhusu Wajumbe wote wa Katiba
kama walivyoaninishwa ktk sheria kuwepo ndani ya Bunge hilo ili kulinda
usawa na haki ya kila mwakilishi.
Kuzuia
utekelezaji wa sheria iliyoaifuta tume ya Kutunga Katiba ili iendelee
kuelimisha Bunge maana na maudhui ya Rasimu ya pili ili taifa lipate
ufahamu unaostahili.
Kuamuru
Serikali kuufungua Mtandao wa Tume ya Katiba uliofungwa ili kuwapa
wananachi wote uhuru na uwezo wa kupata ufahamu wa mengi yaliyozuiwa
wasiyajiue baada ya tovuti hiyo kufungwa.
Kutoa
kinga kwa Vyombo vya Habari vinavyolenga kuendesha mijadala ya Wazi
katika kuelimisha wananchi kuhusu maudhui ya ufahamu wa Rasimu ya 2 ya
Katiba ili waweze kujiandaa kwa ufahamu ufaao kuelekea upigaji wa Kura
kama hatua hiyo itafikiwa.
Kutoa
tafsiri Kamili ya misingi ya Rasimu kulingana na sheria ya Katiba, na
kuhakikisha misingi yake mikuu ya Rasimu ya 2 (ambayo yanatokana na
maoni ya Umma) haiguswi au kumomonyolewa au kuvurugwa kwa hila na
makundi ya wachache wanaoongozwa na Spika.
Kutoa
kinga kwa waliokuwa wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Katiba waendelee
kuelimisha wananchi ktk makongamano ya wazi na kuwaongezea ufahamu zaidi
maana Rasimu hiyo ndio msingi wa Katiba yao waliyoiomba kwa miaka zaidi
ya 30.”
Kama
TLHRC na JUKATA wanaipata hii, watoe ‘what’s next’ ili wananchi wajue
hatma ya haki na maoni yao, ili isiwe too late, na kuwa endapo itaachiwa
Katiba itakayoundwa na wachache ikamilike, itakuwa ndio msingi na
chanzo cha matatizo makubwa zaidi kitaifa ambayo yangeweza kuwekwa sawa
na mahakama mapema kwa sasa!
Nawasilisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni