Jeshi la Iraq likishirikiana na
wanamgambo wa madhehebu ya ki-shia pamoja na wapiganaji wa ki-kurdi
limeanzisha mashambulizi makali ili kujaribu kuwakabilia wapiganaji wa
Islamic state ambao wameuzunguka mji wa Amerli.
Wakati huohuo idara ya ulinzi nchini Marekani
imesema kuwa ndege za kijeshi za marekani imeangusha misaa ya
kibinaadamu katika mji wa Amali uliozungukwa na islamic state.Duru kutoka mji wa Tuz Khormutu zimeiambia BBC kwamba vikosi vya muungano vinashambulia kutoka kusini na kazkazini.
Zimeongezea kuwa oparesheni hiyo hailengi kuwaondoa wapiganaji hao pekee bali pia inajaribu kuifungua barabara kuu kati ya Baghdad na kazkazini mwa taifa hilo.
Wakati huohuo wanajeshi wa Marekani wametekeleza mashambulizi zaidi ya angani dhidi ya wapiganaji wa Islamic state karibu na bwawa la Mosul kazkazini mwa Iraq.
Idara ya Ulinzi nchini Marekani Pentagon imesema kuwa ndege za kijeshi pamoja na zile zisizokuwa na rubani ziliharibu magari saba ya kivita yanayotumiwa na wapiganaji wa Islamic State.
Imesema kuwa oparesheni hiyo ni ya kuwaunga mkono wanajeshi wa Iraq na wapiganaji wa kikurdi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni