WATU kumi wakiwemo watoto wawili
wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika
ajali iliyohusisha magari mawili.
Ajali
hiyo imetokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya
abiria maarufu kama daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina ya
Toyota Hiace na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158
CSV.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo
ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea
Mbalizi kulivaa lori lililokuwa likiingia barabarani.
Walisema
inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka
mlima mkali wa Mbalizi ingawa pia walimtupia lawama dereva wa lori
ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Lori lenye namba za usajili T 158 CSV lililoparamiwa na daladala.
Askari wa usalama wa barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo.
Eneo ambalo daladala hiyo iliyofumuka.
Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea.
Lori hilo baada ya ajali.
Hivi ndivyo daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyoharibika baada ya ajali hiyo.
Mashuhuda wakiwa wameizunguka daladala hiyo kushuhudia kllichotokea.
Hapa ndipo eneo ambapo ajali imetokea, askari wa usalama barabarani wakiendelea kufuatilia ajali hiyo.
Ilikuwa ni ajali mbaya.
Mashuhuda.
Muuguzi
Mkuu wa Hospitali Teule ya Ifisi, Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako
majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7
ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.
Alisema
kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa
Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huku wengine wakiendelea
kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na wanawake wanne na wanaume wanne.
Hata
hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja
kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo dereva wa lori alitokomea mara
baada ya tukio.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni