‘Aliweka saini kabisa ya kukataa kufanyiwa opareshen ili ajifungue kwa kutumia njia hiyo hivyo ikabidi ajifungue kwa njia ya kawaida ambayo ilimfanya atokwe na damu nyingi sana na ndicho kilichosababisha kifo chake’ hizi ni sentensi za mwanzo kutoka kwa Dr. Baraka Malegesi wa hospitali ya Bugando ambao ndio imewahifadhi hawa watoto kwa sasa.
Akihojiwa na millardayo.com Dr. Malegesi ameendelea kusema ‘tumewapokea watoto na bado tuko nao hapa tunawahudumia vizuri wako na mama yao mdogo lakini hali ni ngumu kwa sababu maisha ni magumu kwake na tumejitolea hospitali kuwapa maziwa lakini gharama ni kubwa kwa sababu wiki ni zaidi ya elfu 70 kuwahudumia sasa katika kipato cha chini ndugu zake hawana uwezo’
Daktari huyu amesema kama kuna Mtanzania yeyote anaguswa kusaidia watoto hawa kwa fedha yoyote ile hata ya kutuma kwa M-Pesa, anaweza kufanya hivyo wakati wowote kwa kumtumia mama mdogo wa huyu mtoto ambae namba yake ni 0767 443112 anaitwa Regina Masalaisengwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni