Mwanamke
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Cecilia Hamis (pichani), mkazi wa
Majoe Mjimpya Relini jijini Dar es Salaam amemlalamikia mumewe
aliyemtaja kwa jina la Hamis Juma kwamba ametembea na mbwa wao mweusi
hadi kumpa mimba.
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, mwanamke huyo alisema alibaini hilo wiki mbili zilizopita.
“Nililigundua
hilo wiki mbili zilizopita. Nakumbuka ilikuwa usiku nikiwa nimelala,
nikamsikia mbwa mmoja (kati ya wawili) analia. Niliamka kwenda kuangalia
ili kujua sababu, kufika nikawasha tochi ya simu, nilishangaa sana
kumwona mume wangu yuko naye anafanya mapenzi.
“Nilimuuliza anachokifanya, akasema anammalizia shida zake kwa kuwa hakuna mbwa wa kiume wa kumsaidia,” alisema mwanamke huyo.
Akiendelea kumlalamikia mume wake kwa madai hayo mazito, mama huyo alisema:
“Siku
iliyofuata usiku tena, nikiwa nimelala nilimsikia mbwa akilia,
nikaamka. Safari hii niliambatana na watoto wangu, tukaenda nje, kufika
tukamshuhudia mume wangu akifanya tukio kama la jana yake, nilipomuuliza
akanipa majibu yaleyale kwamba anammaliza shida zake mbwa huyo.”
Akaendelea: “Hawa
mbwa waliletwa wawili wakiwa wadogo kabisa na wote ni majike na tangu
walipoletwa sijawahi kumwona mbwa dume hata siku moja kwani mara nyingi
tunawafungia kwenye banda lao.
“Na tangu mume wangu aanze mchezo huo huyo mbwa mmoja mweusi (pichani) amenawiri kupita kiasi, naamini amempa mimba.”
Mwanamke
huyo alisema kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo, aliamua kuwaeleza
majirani ambao nao walimshauri aende kuripoti kwa mjumbe wa eneo hilo.
Akizungumza
na Uwazi, Mjumbe wa Shina Na. 26, Majoe Mjimpya, Mbaruka Nyamaishwa
alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mwanamke huyo akamshauri
kuyapeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari.
Habari
zaidi zinawekwa wazi kwamba, majirani nao walipoona mwanamke huyo
anachelewa kwenda polisi, wao walimsomba na kwenda naye ambapo walitoa
taarifa katika Dawati la Jinsia.
Mkuu
wa dawati hilo, Koplo Golbert aliongozana na walalamikaji hao hadi
nyumbani kwa mdaiwa ambapo alimkagua mbwa huyo na kuwaamuru wanandoa hao
kuripoti kwenye kituo hicho cha polisi bila kukosa jana Jumatatu saa 3
kuonana na mkuu huyo na uchunguzi kuendelea.
Uwazi
lilimuuliza swali moja mwanamke huyo, ni kwa nini anasema aliamka na
kutoka nje usiku bila kueleza mumewe anakuwa wapi muda huo kwani
hakuonyesha kushangaa kutomwona kitandani?
Anajibu: “Tulitengana vyumba kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia.”
Uwazi lilimgeukia mume wa mwanamke huyo na kumuuliza kuhusu madai mazito ya mkewe ambapo alisema:
“Mimi
sijawahi kufanya kitendo hicho na mbwa ila nahisi mke wangu na hawa
majirani wa hapa wananitengenezea hilo tukio ili nikafungwe jela maisha,
halafu wao waweze kuchukuwa mashamba yangu kwani ndani ya ndoa yangu
kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara.”
Uwazi
lilitilia shaka uwezekano wa mbwa kunasa mimba ya binadamu, hivyo
lilimsaka daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na
kumuuliza kuhusu madai ya mwanamke huyo.
Msikie: “Mh! Binadamu kumpa mimba mbwa haiwezekani. Binadamu anaweza kumpa mimba sokwe, kwa mbali sana nyani. Lakini si mbwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni