Mwili wa Marehemu Dk. Sengondo
Mvungi ukifanyiwa maombi mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Wanachama wa NCCR-Mageuzi wakiwa
wamelibeba sanduku lililohifandhi mwili wa kiongozi huyo wa NCCR-Mageuzi
na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya.
Waombolezaji waliofika uwanjani hapo kuupokea Mwili wa Dk. Mvungi.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiwa uwanjani hapo.
Baadhi ya waombolezaji waliofika uwanjani hapo.
Mjane wa Marehemu, Bi Anna Mvungi akiwa uwanjani hapo kuupokea mwili wa mumewe
Ndugu wakilia kwa uchungu...
Na Mdadisi Mambo Blog
Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Marehemu Dk. Sengondo Mvungi umewasili nchini kutoka Afrika Kusini.
Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Marehemu Dk. Sengondo Mvungi umewasili nchini kutoka Afrika Kusini.
Makumi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ndugu
jamaa na marafiki wa Marehemu dk. Sengondo Mvungi walifika uwanja wa Ndege wa Mwalimu
Julius Nyerere upande wa Mizigo na kuupokea mwili wa kiongozi huyo na mwana familia.
Mapokezi ya mwili wa Dk. Mvungi aliyefariki juzi
kufuatia majeraha ya shambulizi la majambazi lililomkuta nyumbani kwake nombemba
2 mwaka huu na kupeleka Nchini Afrika Kusini kwa Matibabu, yaliongozwa na Mkewe
mama Anne Mvungi.
Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde
Warioba, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Sengondo Mvungi, Mwenyekiti wa NCCR-Magezi, na
wajumbe takriban wote wa tume ya mabadiliko ya Katiba mpya.
Sanduku hilo lilifunikwa bendera ya Chama cha NNCR-Magezi.
Mwili wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi unataraji kuagwa
kesho katika viwanja vya Karimjee kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini Kwao Kisangara
juu, Wilaya ya mwanga mkoani Kilimanjaro kwa Maziko siku ya jumatatu.
________________
MUDA
|
TUKIO
|
LEO, NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK
NYERERE
|
|
Saa 12:50 jioni
|
Kuwasili kwa
mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN
|
KESHO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE
|
|
Saa 2:00 – 3:30
asubuhi
|
Kuwasili kwa
Wageni, Wananchi na Waombolezaji
|
Saa 3:30 asubuhi
|
Kuwasili Mwili
wa Marehemu
|
Saa 4:00 – 5:45 asubuhi
|
Ibada ya Misa
Takatifu, Viwanja vya Karimjee
|
Saa 5:45 – 6:55
mchana
|
Salaam za
Rambirambi na Neno la Shukurani
|
Saa 6:55 – 8:40
Mchana
|
Kuaga Mwili wa
Marehemu
|
Saa 9:00 Alasiri
|
Msafara kupeleka
mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi
|
KESHO KUTWA, NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU
- KIBAMBA, MSAKUZI
|
|
Saa 2:30 – 4:30
asubuhi
|
Ibada ya Misa
nyumbani kwa marehemu
|
Saa 5:00 asubuhi
|
Kuanza safari ya
kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni