Diamond
Platinumz ambaye jina lake halisi la dini ya kiislamu ni Naseeb Abdul
ameshambuliwa Instagram na baadhi ya mashabiki baada ya kupost picha
akiwa beach huko ughaibuni huku ameshikilia kamba iliyomfunga mbwa.
Mashabiki
wengi walimshambulia wakielekeza point yake kwenye suala la imani ya
dini ya kiislamu huku wakiunganisha tukio hilo na mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
Rashyalhambeshy:
ramadhan acha kupost pc zisizo eleweka ww umaaruf ww una umaaruf km
mtume muhammad s.w.a na yote kakataza acha mambo yk ayo jua kuna kufa
muangalie firauna laanatullah ila me lng jicho. na ktk dini tumeambiwa
tukumbushaneni me nimekemea kwa mdomo ok.
Hata
hivyo sio wote waliomshambulia, wapo wengi pia waliomtetea kwa points
tofauti kama Leanlilie aliyetumia point hiyo hiyo ya imani.
leanlilie :I
jus keep wondering who a u to judge another person?kumhukumu mwenzio
tuu ni dhambi wew je ni mwema sana?huu ni wakati wa toba jisalie na
uombee makosa yako,mwachie Allah ndio mtoa hukumu we Tanzanians tumezidi
jaman khaaaaa!!can we atleast think abt our sins and pray acheni watu
ma maisha yao.!
Nimejaribu
kuwauliza watu wawili watatu ambao wamejikita katika masuala ya dini ya
kiislamu kuhusu picha hiyo na imani ya dini hiyo, lakini wao
wamenieleza kuwa sio kosa kumgusa mbwa bali ni haramu mbwa kumnusa muumini wa dini ya kiislamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni