.

Jumapili, 6 Julai 2014

HRW yanyooshea kidole cha lawama jeshi la Congo na kikosi cha Monusco


DRC-MONUSCO-HRW-Haki za binadamu - 
Makala iliyochapishwa tarehe : Ijumaa 04 julai 2014 - Taarifa za ivi karibuni : Ijumaa 04 julai 2014
Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Congo (Monusco) wakipambana dhidi ya makundi ya waasi..
Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Congo (Monusco) wakipambana dhidi ya makundi ya waasi..
REUTERS/Kenny Katombe

Na RFI
Shirika la kimataifa linalo tetea haki za binadamu lenye makao yake makuu nchini Marekani la Human Right Watch limelituhumu jeshi la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo la FARDC pamoja na vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini humo Monusco kwa kupuuzia kuzuia kutokea kwa machafuko ya mwezi uliopita huko mashariki mwa DRCongo.

Shirika hilo limesema majeshi ya Congo na yale ya Monusco hayakuingilia kati ili kukomesha machafuko yaliogharimu maisha ya watu zaidi ya 30 na ambayo yalitokea katika kijiji cha Mutarule katika usiku wa Juni 6 kuamkia Juni 7 katika mkoa wa Kivu ya Kusini

Mkuu wa ofisi ya MONUSCO wilayani Uvira, Ould Mohamed El Hacen (amevaa shati nyeupe) akiwa na jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz, mbele ya moja ya nymba ziliyochomwa moto katika machafuko ya kikabila yaliyotokea Mutarule, mkoani Kivu Kusini..
MONUSCO / Laurent Sam Oussou
Shirika hilo limeendelea kuwa wanajeshi hao waliwaacha wananchi wa Mutarule waendelee kuuawa wakati ambapo kulikuwa na taarifa za kutokea kwa machafuko hayo na ambapo wananchi waliomba msaada tangu tu yalipoanza machafuko hayo na walikuwa karibu wangeliweza kuingilia kati.
Hivi karibuni kiongozi wa majeshi ya Monusco nchini DRCongo Martin Koble alibaini maskitiko yake kuona vikosi vya Umoja wa Mataifa vilishindwa kuziia mauaji hayo yasitokei.

Wanajeshi wa kikosi cha Monusco wakishirikiana na wanajeshi wa Congo FARDC kwa kuyasaka makundi ya waasi mashariki mwa Congo.
RFI/LL.Westerhoff
Shirika hilo limesema hakuna muhusika hata mmoja wa mauaji hayo aliyekamatwa, hivyo Human rights watch limeilitolea wito jeshi la FARDC na Umoja wa Mataifa nchini DRCongo Munusco kuchunguza nini kilichotokea na kuhakikishi mauaji kama hayo hayatokei

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni