Jumamosi, 21 Septemba 2013
WAKE WENZA WASHIKANA UCHAWI HUKO KIMARA...!!
WANAWAKE wawili walioolewa katika familia moja ‘wake wenza’, mama Hashimu na mama Fadhila, wakazi wa Kimara King’ong’o jijini Dar, hivi karibuni walifikishwa serikali za mtaa kwa kosa la kutukanana matusi ya nguoni pamoja na kushikana uchawi.
Inadaiwa kuwa wanawake hao ‘walimwagiana’ matusi hayo usiku wa manane na kusababisha watu wengine kukosa usingizi na kukusanyika kuwasikiliza.
Mara baada ya kufikishwa serikali ya mtaa, wake wenza hao walitakiwa kueleza ugomvi wao na kila mmoja kuanza kushusha tuhuma kwa mwenzake.
Mapaparazi wetu waliwashuhudia wakati wake wenza hao walipokuwa wakijieleza mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ong’o, Demetrius Mapesi na Mtendaji wake Amina Rashid.
Mama Hashimu alianza kuelezea kisa kizima na kufuatiwa na mama Fadhila ambaye wakati akijieleza alipandisha mori kiasi cha kumfanya atake kumrukia mwenzake.
“Unajua nasikia hasira sana kwa sababu mama Fadhila ameniita mchawi huko mtaani unadhani mimi nitaelewekaje? Ukweli kauli hiyo inaniuma sana,” alisema mama Hashim na kuangua kilio.
Hata hivyo, baada ya kila mmoja kueleza ya moyoni, mwenyekiti wa serikali za mtaa pamoja na mtendaji wake, waliwaamuru wake wenza hao kupeana mkono na kuombana msamaha.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni