.

Alhamisi, 26 Septemba 2013

Watu 15 Wakiwemo Watoto 13 Wamekufa Maji Katika Ziwa Tanganyika


Watu 15 wakiwemo watoto 13 wamekufa maji katika Ziwa Tanganyika, baada ya mtumbwi mkubwa waliokuwa wakisafiria kutoka kwenye kijiji cha Kipwa katika wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa , kuelekea katika kijiji cha Kapele kufuata huduma za kliniki kupinduka ndani ya ziwa hilo.

Akiongea na Itv mganga mkuu wa Wilaya ya Kalambo Dakta Hosea Mang'ombe, amesema kufuatia kijiji cha Kipwa kilichoko kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika kukosa huduma ya zahanati, wananchi wa kijiji hicho wamejiwekea utaratibu wa kupata huduma hiyo kwenye kijiji cha Kapele kilichoko umbali wa zaidi ya kilonita 10, na ndipo walipokumbwa na balaa hilo ambapo pia wanahisi kuwepo kwa mama mjamzito ambaye hadi sasa hajaonekana .
akithibitisha kuhusu tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda, amesema jeshi hilo linaendelea kuchunguza juu ya ajali hiyo mbaya, na kutafuta miili ya baadhi ya watu ambao walikuwa hawajapatikana bado hadi sasa.
Source ITV

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni