.

Alhamisi, 26 Septemba 2013

CHADEMA yapata pigo kubwa wilayani Handeni.Mwenyekiti, katibu na wanachama 380 wahamia CCM


Uongozi wa juu wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Handeni Mkoani Tanga umekihama Chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wilaya na Katibu wake pamoja na wanachama 380 ambao wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)..

Tukio hilo linalotoa taswira mbaya kwa CHADEMA na ishara njema kwa CCM limetokea juzi katika kata ya Kwamatuku, ambapo Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Bulembo alifanya mkutano wake wa hadhara na kupokea wanachama hao wapya wa CCM kutoka CHADEMA.

Viongozi hao wa Chadema ni pamoja na Mwenyekiti wa wilaya ya handeni, Luka Selemani, mwenyekiti wa kitongoji cha maguruwe, mjumbe wa Baraza Kuu Taifa (Chadema) na Mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya wilaya.

Wengine ni Katibu wa wilaya hiyo, Athumani Ngido ambaye pia ni mjumbe wa baraza kuu Taifa na mwenyekiti wa kamati ya utendaji wa Mkoa wa Tanga., Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya wilaya hiyo, Jack son Fransis ambaye pia ni mwenyekiti wa kata ya Kabuku na mgombea udiwani wa Kata hiyo...

Mbali na hao, wamo Mwenyekiti wa Tawi la umoja wa Vijana wa Tawi la Kwamatuku, Abrahaman Mtengwa na mjumbe wa kushughulikia migomo ya chama hicho, Juma Mkomba..

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara, Bulembo alisema kukimbia kwa viongozi na wanachama hao ni ishara kuu ya chama hicho kusambaratika vipande vipande katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu...

Alisema kadiri siku zinavyokwenda Chadema kitazidi kusambaratika kutokana na baadhi ya viongozi wake kukumbatia madaraka huku wengine wakiachwa kuwa wapiga debe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni