BONGONEWZ255
KWA MATANGAZO 0718761696
Pages
HOME
contacts
TANGAZA NASI BIASHARA YAKO
.
Jumatatu, 30 Septemba 2013
VIDEO: POLISI WATUMIA NGUVU KUWATAWANYA WANANCHI WALIOKUWA WAKIIBA MAFUTA BAADA YA LORI KUPINDUKA....
Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro wamelazimika kutumia nguvu kuwatawanya wananchi na kuwachapa viboko watu waliokuwa wakiiba mafuta mara baada ya ajali la lori liliosheheni mafuta aina ya Dizel lililokua likitokea jinini Dar es Salaam kuelekea Zambia kupinduka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro.
ITV imeshuhudia baadhi ya wananchi wakiwa na ndoo na madumu huku kukiwa na mvutano mkubwa kati yao na polisi ambapo wananchi hao wametupia lawama askari wa jeshi la polisi kuwafukuza kwa madai kuwa hawaoni sababu kwani kuanguka kwa gari hiyo imekuwa ni fursa kwao.
Nae mkuu kituo cha usalama barabarani mkoa Morogoro wa Leonard Fungu akizungumzia tukio hilo amesema wamelazimika kutumia nguvu kuwatawanya wananchi waliokuwa wakiiba mafuta kwani wizi wa mafuta kwenye matukio ya ajali si kitendo cha uungwana pia wanaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao.
Ajali hiyo imetokea wakati dereva wa lori alipokuwa akikata kona . Gari lilimshinda na kupinduka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni