Jumatano, 25 Septemba 2013
Mbinu za Magaidi kulipua bomu Darajani Zanzibar ZAKWAMA
Watu wasiofahamika bado, usiku wa kuamkia jana Jumatatu walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa bomu lililokuwa katika mfano wa 'sausage' karibu na eneo la biashara kando ya Barabara ya Darajani mjini Zanzibar.
Msaidizi wa Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mkadam Khamis Mkadam akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kuhusu taarifa hiyo alisema, mlinzi binafsi, Amour Kassim Amour (36), aliyekuwa kazini kwenye Duka la Sahara, aliona idadi ya watu katika gari aina ya 'pickup' wakitokea Bwawani kuelekea Mkunazini, walikwenda uelekeo wa dukani alipokuwa akilinda, na walipofika hapo walipunguza mwendo, ndipo mmoja wao aliporusha guruneti upande wake, na kitu hicho kilitua katikati ya masanduku yaliyokuwa mbele ya duka hilo.
"...lilikuwa likitoa moshi. Kwa ushujaa, Amour aliliokota na kulitupa mbali na maduka," "Kwa bahati, Amour alilitupa kwenye uwanja wa wazi na hakukuwa na wanunuzi katika mtaa huo wenye shughuli nyingi kwa sababu ilikuwa ni usiku," alisema Mkadam akiongeza kwamba guruneti lililipuka kwa mlipuko wenye sauti kubwa dakika chache baadaye.
Polisi walifanikiwa kupata mabaki ya unga unga na kukusanya kokoto zilizotokana na athari ya mlipuko huo.
Polisi wameanzisha msako na uchunguzi katika tukio hilo, na kuwataka Wazanzibari kuwa watulivu na kuripoti kitu chochote kinachoshukiwa
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni